Nilivuta sigara tangu mtoto, acheni haina maana- Thierry
Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, simulizi ya mtu aliyeanza kuvuta sigara akiwa kijana balehe na sasa ameamua kuacha inamulika ni kwa nini shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO linasisitiza umuhimu wa kampeni za kuacha tumbaku kwani ni miongoni mwa visababishi vikubwa vya maambukizi ya saratani ya mapafu inayooongoza kwa kuua zaidi vifo miongoni mwa wanaume duniani.