ICCAO Tanzania: Shirika la vijana linalosaidia kufanikisha SDGs nchini Tanzania
Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani yamekuwa uwanja wa wazi kwa wadau kutoka kila pembe ya dunia kuja katika mikutano mbalimbali na kubadilishana uzoefu.