Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mama akiwa amembeba mwanae mwenye umri wa miaka miwili huko nchini Côte d'Ivoire, na aligundua kuwa hakuwa na VVU wakati amebeba ujauzito
© UNICEF/Frank Dejong

Mwongozo mpya wazinduliwa kuhusu VVU na UKIMWI: Kuna matumaini makubwa

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, hii leo limezindua mwongozo wa kisayansi na kimaadili kuhusu Virusi Vya Ukimwi, VVU au HIV vinavyosababisha UKIMWI au AIDS, mwongozo ambao pamoja na mambo mengine unafafanua ni kwa jinsi gani matumizi sahihi na ya wakati wa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI yanaweza kuondoa hatari ya anayeishi na VVU kuambukiza kwa mpenzi wake au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Jamaa wakisubiri nje ya hospitali moja huko Kassala, Sudan, ambapo dada yao mwenye umri wa miaka 28 anatibiwa homa ya dengue. (Maktaba)
OCHA/Saviano Abreu

Nusu ya watu duniani hatarini kuugua Dengue: WHO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limesema takriban nusu ya idadi ya watu ulimwenguni hivi sasa wapo hatarini kuungua ugonjwa wa Dengue huku ikikadiriwa kila mwaka watu kati ya milioni 100 mpaka 400 wanapata maambukizi.

Sauti
2'35"
Susan Auma Mang’eni (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirika na Biashara ndogondogo wa Kenya akihojiwa na Flora Nducha katika Makao Makuu y aUmoja wa Mataifa, New York Marekani.
UN News

Serikali imesikia kilio chenu Wakenya ina mikakati chonde chonde kuweni na subira: Susan Mang’eni

Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF limekunja jamvi jana hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani baada ya siku 10 za tathimini ya utekelezaji wa malengo hayo au SDGs. Waakilishi wa nchi na serikali, wanazuoni, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wanaharakati na vijana ni miongoni mwa waliohudhuria, na Kenya haikubaki nyuma katika jukwaa hilo.

Sauti
3'6"