Tuhakikishe watu ni msingi wa kila jambo tunalofanya 2019- Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaja maeneo matatu ya utekelezaji kwa mwaka huu wa 2019.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaja maeneo matatu ya utekelezaji kwa mwaka huu wa 2019.
Mahakama ya kimataifa ya makossa ya jinai, ICC leo imemwachia huru rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo na aliyekuwa mkuu wa vijana Charles Blé Goudé baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha pasipo shaka mashtaka yote dhidi yao. Arnold Kayanda na taarifa zaidi.
Dau la kijadi lililotengenezwa na taka za plastiki zilizookotwa pwani ya Kenya na miji mbalimbali litaanza safari yake ya kwanza tarehe 24 mwezi huu kutoka mji mkongwe wa Lamu nchini Kenya hadi mji mkongwe huko Zanzibar nchini Tanzania tarehe 7 mwezi ujao, ikiwa ni safari ya umbali wa kilometa 500.
Nchini Nigeria, Kuongezeka kwa mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi yaliyojihami kaskazini mashariki mwezi uliopita wa Desemba na kumesababisha watu wengi zaidi kufurushwa makwao kutoka eneo la Baga na kuelekea kwenye kambi za wakimbizi wa ndani hujo Maiduguri na Manguno ambako tayari kuna msongamano. John Kibego na taarifa zaidi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetangaza leo kuanza kwa kampeni ya kimataifa ya watu kutembea na kufikisha umbali wa kilometa bilioni 2 ambazo wakimbizi hulazimika kutembea kila mwaka. Taarifa zaidi na Arnold Kayanda.