Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mtaalamu wa Haki za Binadamu anahimiza nchi maskini zisamehewe madeni

Dktr Cephas Lumina, Mtaalamu Maalumu wa UM juu ya Haki za Binadamu juu ya athari za madeni kwa ustawi wa uchumi wa nchi zinazoendelea alinakiliwa kwenye ripoti alioitoa kabla ya Mkutano wa Doha, utakaofanyika katika siku za karibuni, ya kwamba Nchi Wanachama zitakazohudhuria kikao hicho zitalazimika kukamilisha juhudi za pamoja za kupunguza mzigo huo wa madeni.~~

Hapa na Pale

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) linajitayarisha sasa hivi kuongeza mara mbili zaidi idadi ya watu watakaohudumiwa chakula mwezi Novemba nchini Zimbabwe; na kwa wakati huo huo WFP imetahadharisha italazimika kupunguza posho ya chakula inayogawa kwa umma Zimbabwe kwa sababu ya upungufu wa fedha za kukidhia mahitaji yao. Hivi sasa WFP imeomba ifadhiliwe na wahisani wa kimataifa msaada wa dola milioni 140, fedha zinazohitajika kuendesha operesheni zake kuanzia kipindi cha sasa hadi mwisho wa Machi 2009. Mnamo mwezi Oktoba, kipindi ambacho WFP ilipoanzisha operesheni zake kubwa za kugawa chakula Zimbabwe, ilifanikiwa kugawa tani 29,000 za posho za chakula kwa umma unaokadiriwa milioni mbili.~

Mkutano wa Nairobi juu ya JKK waamrisha mapigano yasitishwe, halan

Mwisho wa wiki iliopita wajumbe waliohudhuria mkutano wa Nairobi ulioandaliwa na Umoja wa Afrika kuzingatia mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, mkutano ambao uliungwa mkono na UM na kuhudhuriwa na KM Ban Ki-moon, walitoa taarifa maalumu ya pamoja, ilioyanasihi makundi yanayohasimiana kusimamisha mapigano yao haraka katika eneo la mashariki na kuyataka yashirikiane kwenye majadiliano ya kusluhisha mvutano wao kwa njia ya amani.

SADC inazingatia kupeleka wanajeshi katika JKK

Wakati huo huo, kwenye kikao cha dharura kilichohudhuriwa na Wakuu wa Taifa na Serikali wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Kusini ya Afrika (SADC), kilichofanyika Ijumapili kwenye mji wa Sandton, Afrika Kusini kulipitishwa mapendekezo kadha, ikiwemo ile rai ya kutuma washauri wa kijeshi kusaidia vikosi vya Serikali kukabiliana na vurugu linaloendelea kutanda katika JKK, pindi Serikali ya huko itatuma ombi la kuhitajia msaada huo. ~