Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hapa na Pale

Shirika la Mchanganyiko la UM/UA juu ya Ulinzi Amani kwa Darfur (UNAMID) limeripoti ile Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Afrika (UA) inayoongozwa na raisi wa zamani wa Burundi, Pierre Buyoya hivi sasa inazuru Darfur. Tume inajaribu kutafuta suluhu ya kuridhisha dhidi ya mfarakano uliopo kati ya Chad na Sudan. Raisi mstaafu Buyoya alisema ana matumaini mema baada ya kufikiwa yale mapatano ya jumla yenye kurahisisha juhudi za kupeleka na kueneza vikosi vya UNAMID katika Darfur.~

Mapigano yafumka Nyanzale baina ya vikosi vya serikali na waasi

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) limeripoti kufumka tena mapigano ziada Alkhamisi asubuhi, katika Kivu Kaskazini baina ya jeshi la taifa, FARDC, na waasi wa CNDP, mapigano ambayo yalitukia kilomita 60 kusini ya eneo la Kanyabayonga, katika sehemu inayojulikana na wenyeji kama Nyanzale.

WFP inaendelea kugawa chakula Goma

Kwa mujibu wa Msemaji wa MONUC ndege ya shehena ya aina ya C130, iliofadhiliwa UM na Serikali ya Ubelgiji, hutua kila siku Goma na bidhaa za chakula za Shirika la WFP, shirika ambalo tangu Ijumatano limeanza kugawa posho ya chakula kwa wahamiaji wa ndani 135,000 waliopo katika zile kambi sita karibu na mji wa Goma.~~

Ukame Ethiopia wahatarisha umma

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imetahadharisha ya kuwa ukame wa muda mrefu ulioselelea nchini Ethiopia sasa hivi unabshiriwa utaendelea katika eneo hilo, mpaka mwakani.

Hapa na Pale

Shirika la Afya Duniani (WHO) limepongeza, na kupokea kwa furaha kuu, azimio la Baraza Kuu la UM liliopitishwa wiki hii liliopiga marufuku kuvuta, na pia kuuza, bidhaa zinazohusika na tumbaku katika maeneo yote ya majengo ya Makao Makuu. WHO imekumbusha matumizi ya tumbaku ndio chanzo kinachoongoza vifo vya maradhi yanayozuilika, hali ambayo husababisha vifo cvya watu milioni tano kila mwaka kutokana na saratani ya mapafu, maradhi ya moyo na magonjwa mebgfineyo. WHO ilisema hata watu wasiovuta sigara walio karibu na wavutaji nawo vile vile wanadhurika kiafya na kitendo hicho.

WFP yaanza kugawa misaada ya chakula katika JKK

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) leo limeanza kugawa misaada ya chakula kwa watu 135,000, ambao walihamishwa makazi kidharura, na hivi sasa wamewekwa kwenye kambi sita za muda za wahamiaji ziliopo kwenye mji wa Goma, katika JKK.

KM atahudhuria mkutano wa UA Nairobi juu ya mgogoro wa JKK

Mkutano maalumu ulioandaliwa na Umojawa Afrika (UA kuzingatia mgogoro wa karibuni katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) utafanyika Ijumaa kwenye mji wa Nairobi, Kenya ambapo wanatarajiwa kukusanyika viongozi wa Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Afrika Kusini pamoja na maofisa kadha watakaowakilisha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.~~