Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Shirika la Mchanganyiko la UM/UA juu ya Ulinzi Amani kwa Darfur (UNAMID) limeripoti ile Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Afrika (UA) inayoongozwa na raisi wa zamani wa Burundi, Pierre Buyoya hivi sasa inazuru Darfur. Tume inajaribu kutafuta suluhu ya kuridhisha dhidi ya mfarakano uliopo kati ya Chad na Sudan. Raisi mstaafu Buyoya alisema ana matumaini mema baada ya kufikiwa yale mapatano ya jumla yenye kurahisisha juhudi za kupeleka na kueneza vikosi vya UNAMID katika Darfur.~

Wawakilishi wa ule mpango wa vijana ulioandaliwa kupinga ubaguzi wa rangi, unaojulikana kama “Mradi wa Sauti za Vijana dhidi ya Ubaguzi wa Rangi na Ukabila”, ulioanzishwa na Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inaripotiwa waliwasilisha mbele ya Bunge la Ulaya mapendekezo kumi ya kuzuia ubaguzi katika tamasha za michezo ya riadha na mashindano. Moja ya mapendekezo yao ni ile rai ya kuchapisha wito dhidi ya ukabila na ubaguzi wa rangi kwenye mikebe ya vinywaji vinavyouzwa katika viwanja vya michezo. Mapendekezo haya yaliibuka baada ya mazungumzo na vijana wa umri baina ya miaka 15 mpaka 18