Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yafumka Nyanzale baina ya vikosi vya serikali na waasi

Mapigano yafumka Nyanzale baina ya vikosi vya serikali na waasi

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) limeripoti kufumka tena mapigano ziada Alkhamisi asubuhi, katika Kivu Kaskazini baina ya jeshi la taifa, FARDC, na waasi wa CNDP, mapigano ambayo yalitukia kilomita 60 kusini ya eneo la Kanyabayonga, katika sehemu inayojulikana na wenyeji kama Nyanzale.

“Kusema kweli, hatujapokea taarifa zozote zenye kuonyesha hisia za wenyeji zimebadilika na ni mbaya dhidi ya MONUC, kwa sababu kila mapigano yanaposhtadi [baina ya makundi yanayohasimiana nchini] watu wameshashuhudia, kihakika, ya kwamba vikosi vya MONUC havipendelei upande wowote, na imedhihirika wazi ya kuwa MONUC ni sio tatizo bali ni sehemu ya suluhu, kwa sababu kila yanapozuka mapigano mapya mwahali pa awali watu wanapokimbilia kupata hifadhi inayofaa ni kwenye pale penye majengo ya MONUC.”