Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

UNHCR imeripoti kupamba uhamiaji mkubwa wa raia Mogadishu

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kufanyika uhamiaji mkubwa wa raia waliong’olewa makazi kwa sababu ya mripuko wa mapigano yaliouvaa mji mkuu wa Usomali, Mogadishu katika siku za karibuni. Ron Redmond, msemaji wa UNHCR aliwapatia waandishi habari Geneva taarifa ziada juu ya tukio hilo kama ifuatavyo:~

Katibu Mkuu apongeza mafanikio ya kikao maalumu cha MDGS

Baada ya mikutano ya ngazi za juu pamoja na warsha kadha wa kadha zilizofanyika siku nzima hapa Makao Makuu, Alkhamisi ya jana, kupitia namna utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) unavyoendelezwa, wajumbe waliowakilisha serikali, taasisi za kimataifa, jumuiya za kiraia na mashirika ya wafanyabiashara waliungana kipamoja na kuitika mwito wa kuchukua hatua za utendaji wa dhahrura ili kupunguza, kwa kima kikubwa, itakapofika 2015, janga la ufukara, njaa iliokithiri, magonjwa yanayozuilika na maafa mengine ya kiuchumi na jamii yenye kusumbua umma wa nchi zinzoendelea.

Hapa na Pale (Taarifa za Kusoma)

UM umeripoti kwamba yale mashirika yanayohudumia misaada ya kihali yameamua kukuza mchango wa dharura katika Usomali ili kuwanusuru maisha watu 15,000 waliong’olewa makazi karibuni katika mji wa Mogadishu, kwa sababu ya mapigano makali yaliofumka kwenye eneo hilo. Inaripotiwa raia 80 waliuawa na mamia wengine walijeruhiwa kwenye uhasama amabo makali yake hayajawahi kushuhudiwa nchini kwa muda wa zaidi ya mwaka na nusu.

Raisi wa Tanzania azingatia umuhimu wa Malengo ya Milenia kukuza maendeleo Afrika

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, kwenye taarifa alioitoa mbele ya wajumbe waliohudhuria kikao cha Baraza Kuu (BK) juu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), alitilia mkazo “umuhimu mkubwa mno” wa mkusanyiko wao. Alikumbusha ya kwamba mnamo tarehe 22 Septemba KM aliitisha mkutano wa ngazi ya juu kuzingatia mahitaji ya kukuza huduma za maendeleo katika bara la Afrika.

Mapitio ya siku ya pili ya majadiliano ya jumla ya Baraza Kuu

Waziri Mkuu wa Uchina Wen Jiabao aliwaamabia wajumbe waliohudhuria kikao cha wawakilishi wote cha Baraza Kuu kwamba sera adhimu ya taifa lake ni kufuatilia njia ya amani kukuza maendeleo,wakati ikijenga nguvu za kijeshi kwa makusudio pekee ya kulinda na kuhami uhuru wake na umoja wa nchi. Alisema Uchina hauna dhamira yeyote ya “kumiliki dunia, si sasa wala si katika siku zijazo.”

Kikao maalumu cha Baraza Kuu kuzingatia utekelezaji wa Malengo ya Milenia

Viongozi wa Mataifa na Serikali zaidi ya 100 wamejumuika asubuhi ya leo kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York kuhudhuria mkutano muhimu, wa kiwango cha juu kabisa, kuzingatia hatua za pamoja za kukomesha umaskini uliokithiri na matatizo ya njaa ulimwenguni, hatua ambazo zilijumuishwa kwenye ule mradi maalumu wa kimataifa uliopitishwa mwaka 2000 ujulikanao, kwa umaarufu, kama mradi wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

KM anahimiza mchango wa dharura kukamilisha MDGs

KM BAN Ki-moon yeye kwenye taarifa yake aliwaambia viongozi wa dunia waliokusanyika kuzingatia Maendeleo ya Milenia ya kwamba wakati umewadia kwa jumuiya ya kimataifa kuingiza nishati mpya ya hamasa kwenye ushirikiano wa kimataifa unaohitajika kuyakamilisha Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) kwa wakati, hasa ikiwa umma wa kimataifa umewania kihakika kupunguza, kwa nusu, umaskini, kutojua kusoma na kuandika na madhara mengineyo ya kiuchumi na jamii yanayosumbua mataifa yanayoendelea. KM BAN aliongeza taarifa yake kwa kukumbusha yafuatayo:~