Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale (Taarifa za Kusoma)

Hapa na Pale (Taarifa za Kusoma)

UM umeripoti kwamba yale mashirika yanayohudumia misaada ya kihali yameamua kukuza mchango wa dharura katika Usomali ili kuwanusuru maisha watu 15,000 waliong’olewa makazi karibuni katika mji wa Mogadishu, kwa sababu ya mapigano makali yaliofumka kwenye eneo hilo. Inaripotiwa raia 80 waliuawa na mamia wengine walijeruhiwa kwenye uhasama amabo makali yake hayajawahi kushuhudiwa nchini kwa muda wa zaidi ya mwaka na nusu.

Mzozo wa maziwa ya unga yalioharibika nchini Uchina, yaliosababisha watoto 13,000 kulazwa hospitali na matatizo ya vijiwe katika figo, ni mgogoro ulioyalazimisha mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa ya WHO na FAO kutoa ilani maalumu yenye kunasihi mataifa kuchukua hadhari ili kuhakikisha vyakula vya watoto ni salama na havijadhuriwa na sumu za kemikali. Maziwa ya unga katika Uchina yaligundulikana kuwa na aina ya kemikali ya melamine, ambayo utomvu wake hutumiwa kwenye vyombo vya kuwekea vitu na katika vitambulisho. Mashirika ya UM yamependekeza kwa kina mama kunyonyesha watoto wao badala yakutumia maziwaya unga, hususankatyika miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa.