Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hapa na pale

KM amelaani mashambulio mawili ya mabomu ya kujitolea mhanga yaliofanyika Alkhamisi katika mji wa Wah, Pakistan, tukio ambalo lilisababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi wingi wa kiraia. Alirudia msimamo wake juu ya vitendo vya kigaidi, vya kihorera, ambavyo alisisitiza ni vya kulaumiwa na na anavipinga kihakika. KM alituma mkono wa huzuni kwa aila ya waathiriwa, Serikali na umma wa Pakistan.

Hifadhi ya makasa wa baharini imetia gia kuu, yasema UNEP

Ripoti iliowasilishwa leo kwenye mkutano unaofanyika Bali, Indonesia kuhusu hifadhi ya makasa wa baharini waliopo kwenye maeneo ya Bahari ya Hindi na Asia ya Kusini-Mashariki, ilibainisha kupatikana maendeleo ya kutia moyo miongoni mwa yale mataifa 27 yaliotia sahihi maafikiano ya kuwalinda wanyama hawa dhidi ya uharibifu wa mastakimu yao.

Hapa na pale

Baraza la Usalama Ijumatano lilikutana tena kusailia tatizo sugu la Mashariki ya Kati, ikijumuisha suala la haki za WaFalastina.~~

Mafuriko Afrika Magharibi yahatarisha afya ya umma

Mataifa ya Benin, Burkina Faso, Niger, Mali na pia Mauritania na Togo yamekabiliwa, sasa hivi, na maafa ya mvua kali zinazobashiriwa kuendelea hadi mwezi Septemba na kuhatarisha afya za mamilioni ya watu wanaoishi kwenye maeno haya ya Afrika Magharibi.