Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC imepongeza kukamatwa afyuni UAE iliovunja rikodi

UNODC imepongeza kukamatwa afyuni UAE iliovunja rikodi

Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Uhalifu na Madawa ya Kulevya (UNODC) imeripoti katika wiki iliopita polisi wa Umoja wa Imarati za Kiarabu (UAE) waliwashika katika Imarati ya Sharjah watuhumiwa 19 wa KiAfghani na kilo 202 za unga wa afyuni iliotakaswa.

Mohamed Abdul-Aziz, Mwakilishi wa Masahariki ya Kati na Afrika Kaskazini wa UNODC alinakiliwa akisema kushikwa kwa wafanyabiashara wa afyuni Shrajah ni tukio la "mafanikio ya taadhima kuu" katika kupiga vita uhalifu unaovuka mipaka wa madawa ya kulevya, na alipongeza polisi ya Sharjah pamoja na Dubai kwa "ujasiri wao, ubingwa wa kazi na ushirikiano na UNODC" kudhibiti jinai kama hiyo.