Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM alaani shambulio la kigaidi Algeria

KM alaani shambulio la kigaidi Algeria

Ijumanne KM Ban Ki-moon alitoa taarifa maalumu ilioshtumu, kidhati, shambulio la kigaidi liliofanyika kwenye mji wa Issers, kilomita 60 mashariki ya mji mkuu wa Algiers, Algeria.

Baada ya taarifa hiyo ya KM kutolewa rasmi UM ulipokea ripoti ziada kwamba gari mbili, zilizoegeshwa mabomu, ziliripuliwa na kuuwa watu 11 Ijumatano (20/08/08) katika mji mwengine wa Algeria wa Bouira. KM ana wasiwasi mkubwa juu ya kukithiri kwa vifo vya raia, tukio ambalo amelishtumu, kwa mara nyengine tena, kuwa amechukizwa nalo hadi na kukumbusha matumizi ya nguvu na vurugu kusuluhisha mizozo na migogoro ni kitendo kisichokubalika katika sheria ya kimataifa. Kadhalika ameitaka jumuiya ya kimataifa kuisaidia Serikali ya Algeria kukabiliana kwa uzito, na kudhibiti vyema tatizo sugu la ugaidi nchini.