Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Operesheni za UM mipakani Ethiopia na Eritrea zasitishwa

Shirika la Kusimamia Ulinzi wa Amani Mipakani Ethiopia/Eritrea, yaani Shirika la UNMEE, limekomesha operesheni zake zote kwenye eneo kuanzia saa sita usiku Alkhamisi, kwa kufuatana na pendekezo la azimio 1827 (2008) la Baraza la Usalama, ambalo lilipitishwa, bila kupingwa, mnamo Ijumatano ya Julai 29 (2008).

BU limeafikiana kuongeza muda wa UNAMID Darfur

Baraza la Usalama Alkhamisi usiku lilipitisha azimio la kuongeza, kwa mwaka mmoja zaidi, muda wa vikosi vya mchanganyiko vya UA na UM katika Darfur (UNAMID) kuendeleza operesheni zao za kulinda amani Sudan magharibi hadi tarehe 31 Julai 2009.

UM unaunga mkono ripoti ya 'CRISIS ACTION' kuhusu Darfur

Wiki hii kundi la mashirika 36 yasio ya kiserekali yanayohudumia misaada ya kiutu katika Darfur, chini ya jina la pampja la \'Crisis Action\', yaliwasilisha ripoti muhimu iliolaumu na kushtumu vikali mapuuza ya jamii ya kimataifa kukataa kuvifadhilia Vikosi Mseto vya UA/UM kwa Darfur vifaa na zana zinazohitajika kuendeleza operesheni zao, kama walivyodhaminiwa na Baraza la Usalama, hasa misaada ya helikopta, askari zaidi na vifaa vyengine vya lazima vyenye uwezo wa kusafirisha vitu na watu kwa urahisi kwenye mazingira magumu ya vurugu katika Darfur. Rodolphe Adada, Mjumbe Bia Maalumu wa Umoja wa Afrika-Umoja wa Mataifa (UA-UM)kwa Darfur alikubaliana na fafanuzi hizo na kuyataka Mataifa Wanachama kutekeleza majukumu yao kwa kulingana na ahadi walizotoa kabla lakini bado kutimizwa.

WHO inahimiza mama wazazi wanyonyeshe watoto wachanga kuwanusuru na maradhi ya utotoni

Kuanzia tarehe mosi hadi 7 Agosti nchi 120 ziada zitashiriki kwenye kampeni maalumu ya kuhamasisha mama wazazi wa kimataifa kunyonyesha watoto, hasa katika miezi sita ya kwanza baada ya kuzaliwa, kipindi ambacho imethibitika maziwa ya mama humsaidia kumpatia mtoto kinga na afya bora dhidi ya maambukizo maututi ya maradhi ya utotoni kama ugonjwa wa kupumua na kuharisha. Kampeni hii imeandaliwa na Shirika la Umoja wa Dunia Kuendeleza Unyonyeshaji (WABA). Miongoni mwa mashirika yanayojihusisha na huduma hii ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) na pia Shirika la Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) wakijumuika na wadau wengine wa kimataifa.