UM unaunga mkono ripoti ya 'CRISIS ACTION' kuhusu Darfur
Wiki hii kundi la mashirika 36 yasio ya kiserekali yanayohudumia misaada ya kiutu katika Darfur, chini ya jina la pampja la \'Crisis Action\', yaliwasilisha ripoti muhimu iliolaumu na kushtumu vikali mapuuza ya jamii ya kimataifa kukataa kuvifadhilia Vikosi Mseto vya UA/UM kwa Darfur vifaa na zana zinazohitajika kuendeleza operesheni zao, kama walivyodhaminiwa na Baraza la Usalama, hasa misaada ya helikopta, askari zaidi na vifaa vyengine vya lazima vyenye uwezo wa kusafirisha vitu na watu kwa urahisi kwenye mazingira magumu ya vurugu katika Darfur. Rodolphe Adada, Mjumbe Bia Maalumu wa Umoja wa Afrika-Umoja wa Mataifa (UA-UM)kwa Darfur alikubaliana na fafanuzi hizo na kuyataka Mataifa Wanachama kutekeleza majukumu yao kwa kulingana na ahadi walizotoa kabla lakini bado kutimizwa.
Sikiliza maelezo ziada kwenye idhaa ya mtandao.