Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Wakulima wa Bukini wanasaidiwa kujitegemea chakula na FAO

Eneo la Bukini mashariki limekamilisha wiki hii mradi maalumu wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) wa kuotesha chakula nje ya majira ya kupanda mbegu, hususan mpunga, mradi uliochukua mwezi mmoja mfululizo kutekelezwa, uliokuwa na makusudio ya kuhakikisha kutapatikana mavuno ya kutosha kukidhi mahitaji ya umma katika siku zijazo, na kwa Bukini kujiepusha kuagizisha chakula kwa wingi kutoka nchi za kigeni, katika kipindi ambapo bei ya chakula imefumka katika soko za kimataifa na nchi masikini huwa zinashindwa kuzimudu bei hizo.

Hapa na pale

Aliyekuwa msemaji wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Yugoslavia ya Zamani (ICTY), Florence Hartmann ameshitakiwa kuiaibisha Mahakama na kudharau madaraka yake kwa madai ya kwamba alifichua, mara mbili, taarifa za siri zinazohusu kesi ya aliyekuwa Raisi wa Serbia, Slobodan Milošović. Hartmann ameamrishwa kuhudhuria Mahakama ya ICTY mjini Hague, Uholanzi Septemba 15, 2008 kusikiliza mashitaka.~

WHO yahadharisha:ukosefu wa usawa unauwa 'halaiki ya umma' kimataifa

Uchunguzi wa miaka mitatu wa Kamisheni juu ya Viashirio vya Afya ya Jamii, uliodhaminiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) wiki hii umewasilisha matukio ya utafiti wao iliobainisha kwamba licha ya kuwa uchumi unaendelea kunyanyuka katika nchi kadha duniani, muongezeko huu wa utajiri wa taifa pekee hausaidii kusawazisha hali ya usawa katika huduma za afya ya umma, kwa ujumla.

BU inashauriana tena kuhusu tatizo sugu la Georgia

Baraza la Usalama la UM lilitarajiwa kukutana kwa mashauriano leo Alkhamisi kusailia hali katika Georgia kufuatia uamuzi wa Shirikisho la Urusi wiki hii kuyatambua majimbo yaliojiengua ya Abkhazia na Ossetia Kusini. Kadhalika wajumbe wa Baraza la Usalama wanazingatia nakala ya awali ya maazimio mawili kuhusu Georgia. ~

UM umekamilisha mafunzo ya polisi kwa Abyei, Sudan

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani kwa Sudan Kusini (UNMIS) pamoja na Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) yamekamilisha mafunzo ya kwanza ya siku 10 kwa polisi wa Abyei, mji ambao umezongwa na vuguvugu la mvutano baina ya makundi ya kaskazini na kusini yalioshiriki kwenye mapigano ya miaka mingi, ya wenyewe kwa wenyewe katika Sudan.

Benki kuu ya dunia inasema umasikini umekithiri ulimwenguni

Benki Kuu ya Dunia imeonya ya kwamba umasikini umekithiri kwa wingi duniani kwa hivi sasa, kinyume na ilivyodhaniwa katika miaka ya nyuma. Benki Kuu imelazimika kurekibisha takwimu zake na sasa inakadiria watu bilioni 1.4, yaani robo moja ya idadi ya watu duniani, huishi kwenye hali mbaya ya umasikini, idadi ambayo ilikiuka makadirio ya nyuma ya watu milioni 985 walioashiriwa kuishi na pato la dola moja kwa siku. ~

Hapa na pale

Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuongeza kwa mwaka moja shughuli za kusimamia ulinzi amani za vikosi vya UM katika Lebanon (UNIFIL). Azimio liliopitishwa, kwa kauli moja, limesema kuenezwa kwa vikosi vya UNIFIL kuendeleza operesheni zake na jeshi lataifa kumesaidia kuandaa “mazingira mapya ya mbinu za kusimamia amani Lebanon kusini.”