Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Wakazi wa Mogadishu wahama mji baada ya mapigano kufumka

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mamia ya jamii za wakazi wa mji wa Mogadishu walilazimika kuhajiri makwao kunusuru maisha katika mwisho wa wiki iliopita, kwa sababu ya kupamba kwa mapigano makali katika eneo hilo. Inakhofiwa uhasama umeibuka katika kipindi ambapo taifa la Usomali vile vile linakabiliwa na ukame mkali ambao ulishuhudiwa mara ya mwisho katika miaka kumi iliopita. Wahisani wa kimataifa waliombwa kufadhilia kidharura misaada ya kihali kwa UM ili iweze kunusuru maisha ya watu milioni 2.5 waliong\'olewa makwao hivi karibuni.

Mkutano wa Durban unazingatia hifadhi bora dhidi ya utumwa mamboleo

Shirika la Kimataifa juu ya Uhamaji (IOM) limeripoti kukutana katika mji wa Durban, Afrika Kusini waundaji sera kadha wa kadha pamoja na viongozi wa serikali kutoka mataifa ya kusini mwa Afrika, kwa madhumuni ya kuzingatia namna ya kuandaa taratibu za kuwakinga raia wanaotoroshwa na kupelekwa mbali na makwao kuhudumia vibarua haramu, mathalan, umalaya au ajira isio ya kulazimishwa isiokuwa na malipo. Mkutano unatarajiwa kuendelea kwa siku tatu.

Mkutano Mkuu wa XII wa UNCTAD kuanzishwa rasmi Accra

Mkutano wa kumi na mbili wa Shirika la UM juu ya Maendeleo na Biashara (UNCTAD) ulifunguliwa rasmi Ijumapili kwenye mji wa Accra, Ghana ambapo wawakilishi 3,000 ziada kutoka serikali wanachama kadha wa kadha, pamoja na wale wanaowakilishia mashirika mbalimbali ya wafanyabiashara na jumuiya za kiraia walihudhuria mkutano.

Ulimwengu unahitajia msukumo mpya kufyeka ubaguzi, anasihi Arbour

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Louise Arbour Ijumatatu mjini Geneva alihutubia moja ya mfululizo wa vikao kadha vinavyoandaliwa na ofisi yake kutayarisha mkutano mkuu wa mwakani utakaofanya mapitio kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Mkutano wa Durban wa 2001 uliokusudiwa kukomesha tatizo la ubaguzi duniani. Arbour aliwaambia wataalamu waliohudhuria kikao cha matayarisho waliohudhuria kikao wa kufyeka ya ofisiyamtatu wakati akizungumzia juu ya matayarisho ya mkutano wa kufuatilia Mkutano wa Durban wa 2001 wa kufyeka ubaguzi duniani, ameshtumu kwamba tangu kikao kilipofanyika wingi wa Mataifa Wanachama yalishindwa kukamilisha mapendekezo ya kukomesha sera za ubaguzi wa rangi kwa sababu zifuatazo.~

Tume ya Kudumu ya Wenyeji wa Asili yakutana Makao Makuu katika kikao cha mwaka

Kikao cha Saba cha Tume ya Kudumu ya UM juu ya Masuala ya Haki za Wenyeji wa Asili, kitakachochoendelea kwa wiki mbili, kilifunguliwa rasmi Ijumatatu, Aprili 21 kwenye Makao Makuu mjini New York. Mada ambayo inatarajiwa kupewa umuhimu zaidi mwaka huu ni ile inayoambatana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye tamaduni maumbile na namna inavyodhuru uwezo wa wananchi wa asili kujipatia riziki za kuendesha maisha.

Kupamba kwa machafuko Ghaza kunamtia wasiwasi KM

Alkhamisi, Michele Montas, Msemaji wa KM aliripoti kwamba KM Ban Ki-moon aliarifu kusumbuliwa na hali ya kuongezeka kwa machafuko katika Tarafa ya Ghaza na sehemu ya Israel kusini. KM alinakiliwa akisema ameingiwa wasiwasi mkuu kuhusu usalama wa eneo kutokana na kukithiri kwa majeruhi wa kiraia kadha wa KiFalastina, wakijumuisha pia watoto wadogo, walionaswa kwenye mapigano na mashambulio ya vikosi vya Israel.

WFP inaomba isaidiwe dola milioni 256 ziada kuhudumia chakula walimwengu

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza mwito maalumu wenye kupendekeza kufadhiliwa na wahisani wa kimataifa dola milioni 265 ziada, ili kukidhi mahitaji ya ule umma muhitaji wenye kuhudumiwa chakula na UM, katika sehemu kadha wa kadha za kimataifa. WFP ilisema msaada huu ziada unahitajika kununua chakula kwenye soko la kimataifa kufuatilia mfumko wa kasi wa bei za chakula uliojiri karibuni.~~

Akiba ya chakula Kenya kuharibiwa na kivu, OCHA yaonya

Ofisi ya UM juu Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba Kenya inakabiliwa kwa sasa na matatizo ya chakula kwa sababu ya kuharibika kwa mavuno ya mpunga yalioambukizwa na wadudu wa kuvu. Elizabeth Brys, Msemaji wa OCHA katika Ofisi ya UM Geneva aliwabainishia waandishi habari Ijumaa asubuhi juu ya tatizo hili:~

Ofisi ya OHCHR kufungwa Angola

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu inatarajiwa kusitisha kazi zake nchini Angola mnamo tarehe 31 Mei, baada ya wenye madaraka katika taifa hilo kukataa kutia sahihi makubaliano ya jumla ya kuanzisha rasmi ofisi ya kulinda na kutekeleza haki za binadamu nchini humo. ~ ~