Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakazi wa Mogadishu wahama mji baada ya mapigano kufumka

Wakazi wa Mogadishu wahama mji baada ya mapigano kufumka

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti mamia ya jamii za wakazi wa mji wa Mogadishu walilazimika kuhajiri makwao kunusuru maisha katika mwisho wa wiki iliopita, kwa sababu ya kupamba kwa mapigano makali katika eneo hilo. Inakhofiwa uhasama umeibuka katika kipindi ambapo taifa la Usomali vile vile linakabiliwa na ukame mkali ambao ulishuhudiwa mara ya mwisho katika miaka kumi iliopita. Wahisani wa kimataifa waliombwa kufadhilia kidharura misaada ya kihali kwa UM ili iweze kunusuru maisha ya watu milioni 2.5 waliong\'olewa makwao hivi karibuni.