Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupamba kwa machafuko Ghaza kunamtia wasiwasi KM

Kupamba kwa machafuko Ghaza kunamtia wasiwasi KM

Alkhamisi, Michele Montas, Msemaji wa KM aliripoti kwamba KM Ban Ki-moon aliarifu kusumbuliwa na hali ya kuongezeka kwa machafuko katika Tarafa ya Ghaza na sehemu ya Israel kusini. KM alinakiliwa akisema ameingiwa wasiwasi mkuu kuhusu usalama wa eneo kutokana na kukithiri kwa majeruhi wa kiraia kadha wa KiFalastina, wakijumuisha pia watoto wadogo, walionaswa kwenye mapigano na mashambulio ya vikosi vya Israel.

Kadhalika, John Dugard, Mkariri Huru Maalumu wa UM anayehusika na haki za Wafalastina wanaoishi kwenye maeneo yaliokaliwa kimabavu na Israel, alitoa taarifa maalumu mjini Geneva kuhusu hali ya Ghaza ambayo iliitaka UM, kwa kupitia Baraza la Usalama, kufanya kila iwezalo kupatanisha makundi yanayohasimiana Mashariki ya Kati, yaani Israel, Hamas na Wafalastina walioshika Madaraka katika eneo la Ramallah. Alisema pindi Baraza la Usalama litashindwa kuyatekeleza hayo, alipendekeza KM atumie wadhifa wake kukomesha hali ya hatari iliovuma kineoe na ambayo huathiri zaidi raia. Alikumbusha kwamba kimaadili UM umekabidhiwa na walimwengu dhamana kuu ya uangalizi pamoja na ulinzi wa mwisho wa haki za binadamu ili kusawazisha haki na amani ya kimataifa.

Mwandishi habari wa Redio ya UM, Samir Imtair, Alkhamisi alimhoji John Ging, Mkurugenzi wa Operesheni za Misaada ya Kiutu za Shirika la UM la UNRWA, ambalo linalohusika na wahamiaji wa KiFalastina. Ging alitupatia fafanuzi zake kuhusu hali halisi, kwa sasa, kwenye eneo la vurugu na mapigano la Ghaza.

Sikiliza ripoti kamili kwenye mtandao.