Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mkutano wa ngazi za juu kuitishwa Makao Makuu kuzingatia Darfur

Ijumaa, Septemba 21, kulifanyika kikao cha faragha kwenye Makao Makuu na kuhuduriwa na wawakilishi kutoka mataifa 26, ikiwemo Sudan, na pia wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama, wawakilishi wa mataifa jirani na Sudan, na wawakilishi wa Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika (AU) pamoja na maofisa wa Umoja wa Ulaya, na wawakilishi wa kutoka Umoja wa Nchi za Kiarabu, halkadhalika.

Mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro alifanya mazungumzo maalumu na Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM ambapo alichukua fursa hiyo kufafanua mwelekeo mpya kuhusu kazi na shughuli za UM duniani. Alisailia juu ya juhudi za KM Ban Ki-moon katika kuharakisha utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), kwa wakati, Afrika kusini ya Sahara. Kwenye makala hii ya awali ya mahojiano yetu Naibu KM Migiro anazugumzia mada mbili: awali, utekelezaji wa Malengo ya MDGs Afrika kusini ya Sahara na, pili, suala la Darfur. ~~Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.

Naibu KM wa UM anasailia matatizo ya kimataifa na Redio ya UM

Wiki hii wasikilizaji Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM ilibahatika kupata fursa ya kufanya mahojiano maalumu na Naibu KM wa UM, Asha-Rose Migiro kwenye studio zetu. Naibu KM Migiro alisailia mada kadha wa kadha zinazoambatana na shughuli za UM, ikijumuisha utekelezaji wa Malengo ya Milenia ya Maendeleo (MDGs)katika mataifa masikini, suala la Darfur, mageuzi katika UM, udhibiti wa mabadailiko ya hali ya hewa na kadhalika.

Kikao cha 62 cha Baraza Kuu chafunguliwa rasmi

Kikao cha 61 Cha Baraza Kuu la UM kilimalizika rasmi tarehe 17 Septemba na Raisi wa kikao kiko hicho, Shekha Haya Rashed Al Khalifa wa Bahrain, kwenye risala ya kuaga, aliyahimiza mataifa wanachama kuendelea kushauriana, ili kusaidia kuimarisha uelewano mwema wa kitamaduni kati ya jamii mbalimbali za kimataifa.

MONUC inasema "vikosi vya Serekali DRC vinakiuka haki za binadamu"

Ripoti ya Shirika la UM la Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) juu ya utekelezaji wa haki za binadamu katika Kongo-DRC kwa Julai imeshtumu vikali vitendo vya wanajeshi wa Serekali, baada ya kuthibitisha kwenye uchunguzi wao kwamba vikosi hivyo vimegunduliwa vikiharamisha haki za binadamu nchini kwa mapana na marefu, ambapo wanajeshi wamekutikana wakiua raia kihorera, wakinajisi wanawake kimabavu, na kuendeleza wizi na dhulma, na kunyanganya raia mali zao.