Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha 62 cha Baraza Kuu chafunguliwa rasmi

Kikao cha 62 cha Baraza Kuu chafunguliwa rasmi

Kikao cha 61 Cha Baraza Kuu la UM kilimalizika rasmi tarehe 17 Septemba na Raisi wa kikao kiko hicho, Shekha Haya Rashed Al Khalifa wa Bahrain, kwenye risala ya kuaga, aliyahimiza mataifa wanachama kuendelea kushauriana, ili kusaidia kuimarisha uelewano mwema wa kitamaduni kati ya jamii mbalimbali za kimataifa.

Siku yapili yake, Ijumanne alasiri tarehe 18 Septemba (2007) kikao cha 62 cha Baraza Kuu kilifunguliwa rasmi na Raisi mpya, Srgjan Kerim wa kutoka iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia ya Macedonia. Kabla ya hapo Raisi Kerim alikutana na waandishi habari na kuelezea ajenda ambayo angelipendelea kuona inazingatiwa na kupewa umuhimu wa hadhi ya juu katika mijadala ya mwaka huu, ikijumuisha zile mada zinazoambatana na udhibiti bora wa taathira za mabadiliko ya hali ya hewa duniani, uwezekano wa kuleta mageuzi ya kuridhisha katika kazi za UM, hatua za kuchukuliwa kuimarisha misaada ya kufadhilia maendeleo ya nchi masikini, na pia alitaka kuona kasi inaongezwa kwenye zile juhudi za kusuluhisha matatizo ya ufukara, na kwenye masuala yanayoambatana na vita dhidi ya ugaidi.