Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la Iran lazonga kikao cha mwaka cha IAEA mjini Vienna

Suala la Iran lazonga kikao cha mwaka cha IAEA mjini Vienna

Mnamo Ijumatatu, 17 Septemba (2007) Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Kinyuklia (IAEA)lilianza mijadala ya wawakilishi wote mjini Vienna, Austria kwenye kikao cha mwaka.

"Nimeingiwa na wasiwasi sana kusikia baadhi ya wahusika fulani, wakipiga makelele ya kutaka kuanzisha vita [dhidi yakwa sauti kubwa kabisa. Kwa mimi ninavyoiona hali ya mambo ilivyo, siamini mayowe kama haya yanawakilisha mwelekeo wa busara. Wakati jamii ya kimataifa inasema ina wasiwasi kuhusu dhamira hasa ya mradi wa mitambo ya nishati ya kinyuklia wa Iran na kushuku una lengo la hatari, sifikiri dhana hii pekee humaanisha hatuwezi tena kulijadilia suala hili kidiplomasiya, kwa taratibu ambazo, hatimaye, zitatupatia suluhu ya kuridhisha!”