Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ameashiria kuwepo 'mwamko wa daraja ya juu' katika Baraza Kuu la mwaka huu

KM ameashiria kuwepo 'mwamko wa daraja ya juu' katika Baraza Kuu la mwaka huu

KM wa UM Ban Ki-moon naye vile vile alifanyisha mkutano maalumu, mwanzo wa wiki, na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu ambapo alisailia mada kadha zinazoambatana na mijadala ya kikao cha 62 cha Baraza Kuu.

"Kikao cha safari hii, ninaamini kitakuwa chenye mhemko mkubwa wa kihistoria kwenye UM. Ilivyokuwa tunasonga mbele na karne ya 21, jamii ya kimataifa imeanza tena kutambua umuhimu wa kulitumia jukwaa la UM kuwa mastakimu halisi ya kujadilia masuala yote yanayohusu amani na ustawi wa kimataifa, na ni mahali pekee ambapo vile vile hugongomelewa suluhu za kuridhisha!”