Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICTR imependekeza kifungo cha muda mrefu kwa aliyekuwa meya Rwanda

ICTR imependekeza kifungo cha muda mrefu kwa aliyekuwa meya Rwanda

Hassan Jallow, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) kwenye hoja za kufunga kesi ya Juvenal Rugambarara, aliyekuwa meya wa Kitongoji cha Bicumbi kuanzia 1993-1994, alipendekeza mtuhumiwa huyo ahukumiwe kifungo cha miaka 12 kwa kushiriki kwenye jinai dhidi ya ubinadamu.

Jallow alisisitiza kifungo hicho ndicho anachostahiki Rugambarara. Timu ya mawakiliwanaomtetea mshitakiwa walipenedekza hukumu ya kifungo ipunguzwe, kwa sababu mashahidi watano wa utetezi walidai kwamba mtuhumiwa Rugambarara aliwahi kutumia wadhifa wake kuokoa maisha ya raia wengi wenye asili ya KiTutsi katika miaka ya 1990.