Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko makali yagharikisha mataifa kadha barani Afrika

Mafuriko makali yagharikisha mataifa kadha barani Afrika

Wiki hii, mafuriko makali yaliripotiwa kufumka na kugharikisha mataifa kadha wa kadha Afrika, kuanzia Mauritania, Afrika Magharibi hadi Kenya, katika Afrika Mashariki, hali ambayo imeathiri sana kihali watu milioni 1.5 kwenye maeneo husika.

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) sasa hivi limo mbioni katika shughuli za kuhudumia chakula pamoja na mahitaji mengine ya kiutu kwa umma muathiriwa uliopo katika sehemu hizo za Afrika, kusini ya Sahara, ziliovamiwa na mafuriko, ikiwemo pia Uganda ambayo inaripotiwa itahitajia msaada wa dharura wa dola milioni 65 kuhudumia kihali watu 300,000.