Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Suala la haki za kibinadamu katika Darfur Kusini

Tume ya wataalamu watano ya Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu ilioatarajiwa kwenda jimbo la Sudan magharibi la Darfur kuchunguza namna haki za kibinadamu zinavyotekelezwa na wenye madaraka, haikufanikiwa kuzuru eneo hilo wiki hii kwa sababu ya kutopatiwa viza na Serekali ya Sudan.

Mtaalamu wa haki za kibinadamu kwa Usomali kuitaka serekali kuachia huru waandishi watatu wa habari

Ghanim Alnajjar, Mtaalamu anayehusika na Haki za Kibinadamu katika Usomali amependekeza na kuawahimiza wenye madaraka Usomali kuwaachia huru, halan, wale waandishi habari watatu wa Kisomali walioshikwa karibuni na kuwekwa kizuizini. Alisema kitendo hiki kinatia wasiwasi na alikumbusha ya kwamba ni muhimu kwa vyombo vya habari kuwa na uwezo wa kueneza ripoti zao bila kuhofu wenye madaraka, msimamo ambao ukitekelezwa kama unavyotakikana ni kadhia itakayosaidia pakubwa kurfufua uslama na amani katika Usomali.

Makundi husika na mzozo wa Darfur yakiri vurugu halizalishi suluhu, wabainisha Wapatanishi wa UM na AU

Jan Eliasson, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Darfur pamoja na Salim Ahmed Salim, Mpatanishi wa Darfur wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU) walikutana wiki hii nchini Sudan kwa mashauriano ya amani na viongozi wa wahamiaji wa ndani ya nchi, majemadari wa makundi ya waasi wasiotia sahihi Itifaki ya Amani ya Darfur, pamoja na machifu wa makabila kadhaa na vile vile wawakililishi wa Sereklali.

Watoto masikini na mayatima Zimbabwe kufadhiliwa misaada ya maendeleo na UM

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) wiki hii limetiliana sahihi na Serekali ya Zimbabwe, pamoja na mashirika 21 yasio ya kiserekali, maafikiano ya kufadhilia jumuiya za kiraia misaada ya kuhudumia uandikishaji ziada wa watoto masikini na mayatima 350,000, ili waweze kuhudhuria masomo ya skuli za msingi. Vile vile msaada huo unatazamiwa kuwahudumia afya na kuboresha lishe watoto husika.

Naibu KM mpya aahidi usimamizi wa kazi za UM kwa nidhamu za fungamano

Ijumatatu, Februari 05 (2007) Asha-Rose Migiro, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo wa Tanzania aliapishwa rasmi kuwa Naibu KM mpya wa UM. Baada ya Bi Migiro kuapishwa na kutia sahihi waraka za UM alijulishwa na KM Ban Ki-moon na waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Naibu KM Migiro aliwaambia wanahabari hawo kwamba atajitahidi kama awezavyo kuziongoza kazi za UM kwa nidhamu iliyoungana, na kwa taratibu zinazoeleweka kwa masilahi na natija za taasisi hii pekee ya kimataifa.