Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wanahitajia misaada ya kihali kusini Afrika baada ya mafuriko haribifu

Maelfu wanahitajia misaada ya kihali kusini Afrika baada ya mafuriko haribifu

Shirika la WFP limeripoti mafuriko haribifu yametanda karibuni kusini ya Afrika na kuathiri maisha na usalama wa makumi elfu ya watu waliojikuta wamenaswa na kuinuka kwa kina cha maji katika maeneo yao,hali ambayo imeangamiza mazao, nyumba na kuchukua maisha ya darzeni za watu.

Mapema wiki ijayo WFP itaanzisha kampeni ya kuihamasisha jumuiya ya kimataifa kuzisaidia juhudi za serekali ya Msumbiji kudhibiti mgogoro huu wa mafuriko na kuipatia misaada ya chakula, huduma za ndege zitakazotumiwa kupeleka misaada ya kihali na kuokoa watu, na pia kusaidia kuwapatia vifaa vya kuwasiliana ili kuboresha operesheni za kupeleka misaada ya kiutu kwenye yale maeneo husika.

Mwaka huu mafuriko yameshaathiri mataifa ya Angola, Bukini, Malawi,Zambia na pia Zimbabwe ambayo yote huhitajia kufadhiliwa misaada ya dharura kukabiliana na janga hili la kimaumbile.