Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku ya Amani ya Kimataifa

Alkhamisi, tarehe 21 Septemba iliadhimishwa na Umoja wa Mataifa (UM), kote duniani, kuwa ni Siku ya Amani ya Kimataifa. Katibu Mkuu Kofi Annan alijumuika kwenye Makao Mkuu mjini New York na watu mashuhuri kadha walioteuliwa na UM kuwa wajumbe wa kuendeleza mbele kampeni ya kuimarisha amani ulimwenguni, akiwemo pia Daktari Jane Goodall, kwenye tafrija za kuiadhimisha Siku hiyo. Daktari Goodall ni mtafiti wa wanyama pori na mtetezi wa hifadhi za mazingira, na ni mtu maarufu Afrika Mashariki ambapo alifanyia tafiti zake muhimu kadha wa kadha juu ya tabia za wanyama pori hususan masokwe.

Serekali ya Uganda kutoa msamaha kwa waasi wa LRA hali ikiruhusu

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uganda, Sam Kutesa aliwaarifu wajumbe wa kimataifa katika Baraza Kuu kwamba serekali yake, ikilazimika, ipo tayari kutoa msamaha kwa viongozi wa kundi la Lord\'s Resistance Army (LRA), kundi la waasi ambalo linajulikana kwa ukatili wa kuwatumia wanajeshi watoto wanaolazimishwa kuendeleza vitendo vya karaha dhidi ya utu, na pia kuendeleza unyanyasaji wa kijinisia dhidi ya wanawake wanaowateka nyara katika Uganda ya Kaskazini. jafanya askari mtoto ambalo limetuhumiwa, katika siku za nyuma, kuendeleza vitendo vya kikatli vilivyoharamisha haki za kiutu dhidi ya watoto na wanawake.

Mikakati ya kupambana na UKIMWI Inahitaji Kubadilishwa

Wanasayansi, wakuu wa mashirika ya kimataifa, wawakilishi wa kiserekali na pia wale kutoka mashirika yasio ya kiserekali waliohudhuria mkutano wa kihistoria juu ya UKIMWI mjini Toronto, Kanada katika mwezi Agosti walitoa mwito uliopendekeza ile mikakati ya kupambana na janga la virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI wenyewe ibadilishwe. A. Aboud kutoka Redio ya UM alihudhuria mkutano huo wa Toronto na alitayarisha ripoti maalumu juu ya pendekezo hilo. Kwa taarifa kamili sikiliza idhaa ya mtandao ya Umoja wa Mataifa.~

Hali katika Darfur, Sudan

KM wa UM Kofi Annan, mnamo mwanzo wa wiki, alishiriki kwenye mjadala maalumu wa Baraza la Usalama uliozingatia hali katika jimbola magharibi la Sudan la Darfur.

UM umetuma wataalamu watatu Cote d'Ivoire kudhibiti kemikali maututi

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Kiutu (OCHA) imetuma timu ya maofisa wataalamu watatu katika Cote d’Ivoire kuisaidia serekali kudhibiti vyema tatizo liliozuka karibuni baada ya kugunduliwa taka za sumu ya kemikali zilizomwagwa mwezi uliopita katika mji mkuu wa Abidjan na kuhatarisha afya na usalama wa raia, kwa ujumla.~