Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

UM kupunguza wahudumia misaada ya kiutu katika Chad

UM umetangaza kwamba kutokana na hali ya usalama inayoendelea kuharibika katika eneo la Chad ya mashariki zile huduma za kupeleka misaada ya kihali kwa wahamiaji wa Sudan 110,000 waliopo huko zitabidi zipunguzwe pamoja na kupunguza wafanyakazi wa UM wanaohusika na kadhia hizo.

Mshoni wa Zambia kutunikwa zawadi ya UM kwa kupiga vita UKIMWI

Jonsen Habachimba, mshoni kutoka Zambia pamoja na shirika linalojulikana kama Jumuiya ya Maendeleo ya Vijiji ya Mboole (Mboole Rural Development) wametunukiwa zawadi ya dola 20,000, ikiwa ni tunzo la awali la UM kwa mashirika ya kiraia yanayojitolea kushiriki kwenye juhudi muhimu za kupambana na UKIMWI.

KM bado anasubiri idhini ya Sudan juu ya vikosi vya mseto vya UM/AU kwa Darfur

KM Kofi Annan alikuwa na mashauriano na Baraza la Usalama wiki hii kuhusu hali katika Darfur,Sudan. Baada ya mkutano wake huo na Baraza la Usalama aliwaambia waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu kwamba Serekali ya Sudan bado haijamtumia jawabu yao ya kuidhinisha maafikiano ya kimsingi, waliokubaliana pamoja wiki iliopita, ya kupeleka vikosi vya mseto vya UM na AU katika Darfur ambayo yanahitajika kidharura kukomesha uhasama na maafa yaliofumka na kutanda kwenye eneo hilo, na kuathiri vibaya maisha ya malaki ya raia.