Skip to main content

Jumuiya ya Kimataifa Yaadhimisha 'Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani'

Jumuiya ya Kimataifa Yaadhimisha 'Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani'

Mnamo 1988 Baraza Kuu la UM lilitoa mwito maalumu uliopendekeza kuutekeleza uamuzi wa Shirika la Afya Dunia (WHO) wa kuifanya tarehe 01 Disemba kila mwaka kuwa ni ‘Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani.’

Hivi majuzi mwandishi habari wa Redio ya UM alizuru Dar es Salaaam, Tanzania na alichukua fursa hiyo kufanya mahojiano na Angela Ramadhani, mratibu wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka mama wajawazito kwa mtoto, anayefanya kazi katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Tanzania.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.