Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wachanga milioni 1.6 hufa kila mwaka kusini ya Sahara - yaripoti UM

Watoto wachanga milioni 1.6 hufa kila mwaka kusini ya Sahara - yaripoti UM

Ripoti ya pamoja kati ya Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF), Shirika la Afya Duniani (WHO) na washirika mengineyo wenzi iliyowasilishwa karibuni kuhusu maendeleo ya afya kwa watoto wachanga imeonya ya kuwa ukanda wa Afrika kusini ya Sahara ndiyo eneo hatari kabisa kuzaa mtoto.~

Kwa mujibu wa ripoti hiyo gharama za kuwastiri asilimia 90 ya mama waja wazito na maafa hayo si nyingi kuzimudu.

Sikiliza idhaa ya mtandao kwa maelezo kamili.