Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Wakulima nchini Rwanda na juhudi za kuimarisha ardhi.
© FAO/Petterik Wiggers

Njaa yashamiri Afrika, waathirika zaidi wakiwa ni Ukanda wa Afrika Mashariki

Idadi ya watu wenye njaa barani Afrika inaendelea kuongezeka, ikichochewa na uwepo wa migogoro, mabadiliko ya tabianchi na kuzorota kwa uchumi sababu nyingine mbalimbali ikiwemo pia janga la COVID-19. Imesema ripoti iliyotolewa leo na viongozi wa mashirika matatu ya kikanda barani Afrika ambayo  yametoa wito wa kuchukua hatua zaidi juu ya mabadiliko ya mifumo ya kilimo.

Sauti
1'56"
Dr. Gladys Kalema-Zikusoka Mshindi wa tuzo ya UNEP kutoka UGANDA
UNEP

Wanakunywa kahawa wakifahamu kwa kufanya hivyo wanaokoa sokwe - Raia wa Uganda mshindi wa tuzo ya UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira duniani, UNEP wiki hii Jumanne ya tarehe 07 limewatangaza washindi wanne wa tuzo yake ya juu kabisa ya mazingira ijulikanayo kama “champions of the Earth Award” kwa mwaka 2021. Mabingwa hao walichaguliwa kutokana na mchango katika mazingira na uongozi wao katika kuendeleza hatua za ujasiri na madhubuti kwa niaba ya watu wengine wa sayari dunia. Dk Gladys Kalema-Zikusoka wa Uganda ni mmoja wa tuzo hiyo ya UNEP katika kipengele cha Sayansi na Ubunifu.  

Sauti
3'39"
Kaimu Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Songelael Shilla
Assumpta Massoi

Siku 5 tu baada ya uhuru wa Tanzania bara, tulijiunga Umoja wa Mataifa na pande zote zinanufaika - Songelael Shilla

Siku kama ya leo tarehe 9 mwezi Desemba mwaka 1961, iliyokuwa Tanganyika au Tanzania Bara ilipata Uhuru wake kupitia mchakato uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa. Siku 5 baadaye, nchi hiyo huru ilijiunga na Umoja wa Mataifa na kuwa mwanachama hadi leo na hii leo inaposherehekea miaka 60 ya uhuru wake, pia inatambua faida inazozipata kwa kuwa mwanachama wa UN kama anavyoeleza Kaimu Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Songelael Shilla alipozungumza na Idhaa hii jijini New York Marekani.

Sauti
2'18"
Wafanyakazi wa UNHCR wanatathmini mahitaji ya watu walioathiriwa na vurugu kati ya jumuiya huko Jebel Moon, Darfur Magharibi.
© UNHCR/John Mwate

Machafuko yanayoendelea Darfur yanatutia hofu kubwa:UNHCR

Machafuko yanayoendelea katika jimbo la Darfur nchini Sudan yamewasababisha maelfu ya watu kufungasha virago na kuyakimbia makazi yao tangu mwezi Novemba mwaka huu, wengi wakitawanywa ndani ya nchi na wengine kwenye mpaka wa nchi Jirani ya Chad limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na kuongeza kuwa linatiwa hofu kubwa na hali hiyo.

Sauti
2'23"