Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Waziri wa afya maendeleo ya jamii wazee na watoto wa nchi hiyo Ummy Mwalimu akizungumza na Flora Nducha wa UN News kandoni mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani kikao cha 63
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya

Bila ushiriki wa wanawake hatutakuwa na Tanzania ya viwanda:waziri Mwalimu

Serikali ya Tanzania imesema bila ushiriki kamilifu wa wanawake haitoweza kutimiza azma ya kuwa na maendeleo ya viwanda itakayoleta tija kwa wote.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa afya maendeleo ya jamii wazee na watoto wa nchi hiyo Ummy Mwalimu akizungumza na Flora Nducha wa UN News kandoni mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani kikao cha 63 kinachoendelea kwenye mako makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani na kuongeza kuwa na huo ndio ujumbe wao pia kwenye mkutano huu

(MAHOJIANO NA UMMIE MWALIM)

Sauti
2'10"
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa amataifa la wanawake-UN-Women,Phumzile Mlambo-Ngcuka,(kushoto) akiwa na wanawake wmjini Baidoa Somalia.
UN Women/Patterson Siema

Hatuwezi kutothamini mchango wa nusu ya watu duniani :Guterres

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo kila mwaka huwa Mach inane wito umetolewa kuhakikisha uwezeshaji wanawake na usawa jinsia vitu ambavyo ni muhimu kwa maendeleo ya dunia. Wito huo umetolewa na viongozi mbalimbali wanawake kwenye Umoja wa Mataifa lakini pia Katibu Mkuu Antonio Guterres. Kaulimbiu ya mwaka huu ikiwa ni “fikra sawa, jenga kwa ufanisi na kuwa mbunifu kwa mabadiliko 

Sauti
3'