Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mtoto wa kiume akiwa ameketi katika kifusi cha nyumba iliyosambaratishwa na kimbunga Rai katika wilaya ya Purok nchini Ufilipino
© UNICEF/David Hogsholt

Madhara ya kimbunga Rai, WFP yaomba usaidizi 

Wiki tatu baada ya kimbunga Odette kinachofahamika kimataifa kwa jina Rai kuharibu eneo kubwa la nchi ya Ufilipino, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP kupitia taarifa yake iliyotolewa hii leo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Manila, limeonya kwamba lishe na uhakika wa chakula viko hatarini katika jamii zilizo katika maeneo yenye hali ngumu ikiwa mahitaji ya haraka ya chakula hayatawafikia katika kipindi cha miezi sita ijayo.

Mwanamke akipimwa Covid-19 katika kliniki huko Palestina
©UNDP/Abed Zagout

Omicron isidharauliwe na kukosa usawa wa chanjo kunatuumiza zaidi - WHO

“Kutokana na kuenea kwa mnyumbuliko mpya wa omicron katika maeneo yote duniani, maambukizi mapya yalifikia milioni 9.5 na vifo vilizidi 41,000 ulimwenguni kuanzia Desemba 27 hadi Januari 2. "Na tunajua kwamba namba hizi ziko chini ya zile halisi." Anaonya Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, Dkt Tedros Ghebreyesus akitoa wito kwa mara nyingine tena kwa usambazaji sawa wa chanjo dhidi ya virusi vya corona. 

Miradi ya IFAD inasaidia kuimarisha Masoko kwa wakulima
Khaled Abdul Wahab

Fahamu namna mkopo wa IFAD ulivyobadili maisha ya wakulima Misri

Mkopo uliotolewa na mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo duniani IFAD nchini Misri umekuwa na manufaa makubwa kwa wakulima wadogo na kutengeneza maelfu ya ajira mpya hali iliyofanya mpaka Bodi tendaji ya IFAD kufunga safari mpaka nchini humo kujionea wenyewe. Anold Kayanda anakuletea taarifa kutoka kwa wakulima wadogo wakieleza namna maisha yao yalivyobadilika. Taarifa ya Anold Kayanda inaeleza zaidi.

Sauti
2'18"