Walinda amani kutoka Tanzania watunukiwa sarafu ya ujasiri na utendaji mzuri

Walinda amani kutoka Tanzania watunukiwa sarafu ya ujasiri na utendaji mzuri
Kapteni Asia Hussein
Walinda amani kutoka Tanzania watunukiwa sarafu ya ujasiri na utendaji mzuri

Walinda amani kutoka Tanzania watunukiwa sarafu ya ujasiri na utendaji mzuri

Amani na Usalama

Walinda amani wanne wa Umoja wa Mataifa kutoka nchini Tanzania wanaohudumu nchini Jamhuri ya Kati wametunukiwa sarafu ya ujasiri na utendaji kazi mzuri. 

Naibu Kamanda wa vikosi ya ulinzi wa Amani nchini humo - MINUSCA Meja Jenerali Maia Pereira amewatunukia walinda amani hao wa TANBATT-5 sarafu maalum ikiwa ni ishara ya kuridhishwa na utendaji kazi wao pamoja na ujasiri katika kutekeleza majukumu yao MINUSCA, na Umoja na Mataifa.

Taarifa kutoka kwa afisa habari wa kikosi hicho Kapteni Asia Hussein aliyeko Bariberati, Magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati inasema wanajeshi hao waliotunukiwa tuzo ni Meja Amulike Nelson Kabale, Kapteni Masoud Petro Mswago, Koplo Ally Swed Mwanamtogole na Private Amin Wilbard Amin. 

Baada ya kukabidhiwa sarafu hiyo meja Amulike Nelson Kabale anasema “Namshukuru mwenyezi Mungu ambaye ndie aliyenifanya kazi yangu hii kuonekana na hii ndio imepelekea kutunukiwa sarafu hii ya ujasiri.Sarafu hii imenifanya kujiamini, kuongeza ujasiri, hari, morali, na uaminifu kwa jeshi la ulinzi la Tanzania, MINUSCA na Umoja wa Mataifa kwa ujumla. Lakini pia limenifanya kutekeleza majukumu yangu ya kuwalinda wananchi wa Jamhuri wa Afrika ya Kati pamoja nakutekeleza majukumu ya Umoja wa Mataifa.”

Walinda amani kutoka Tanzania watunukiwa sarafu ya ujasiri na utendaji mzuri
Kapteni Asia Hussein
Walinda amani kutoka Tanzania watunukiwa sarafu ya ujasiri na utendaji mzuri

Naye Kapteni Masoud Petro Mswago amesema “sarafu hii kwangu ni kitu kikubwa sana kwakufikia hatua ya kutambuliwa kwa utendaji kazi na uongozi wa juu kabisa wa Umoja wa Mataifa MINUSCA hapa nchini CAR. Nishani hii inanipa chachu kuongeza bidii, weledi na uchapakazi katika majukumu yangu kadri mwenyezi Mungu atakavyoniwezesha.”

Meja Jenerali Pereira baada ya kuwatunukia sarafu hizo maalum amewapongeza walinda amani hao ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu walipowasili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.