Hatua zichukuliwe kuondoa madanguro kwenye kambi za wakimbizi- UN
Kufuatia kuwepo kwa ripoti za ubakaji na biashara ya ngono kwenye kambi za wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Naibu Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo ambaye pia ni Mratibu wa masuala ya kibinadamu Bruno Lemarquis ameongoza ujumbe wa mabalozi kutoka nchi za nje kwenye ziara katika moja ya kambi hizo huko Kivu Kaskazini kukutana na wakimbizi. Shuhuda wetu ni Byobe Malenga, mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini DRC.