Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Afya Duniani: Walinda amani wa UN kutoka TZ nchini DRC waadhimisha kwa vitendo

Wakati wa siku ya afya duniani 7 Aprili 2023, walinda amani wa UN kutoka kikosi cha Tanzania cha kutoa msaada wa haraka, TANZQRF katika kwneye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO nchini DRC  wametoa huduma za kupima magonjwa yasiyo ya ku…
TANZQRF3/Methew Makoba
Wakati wa siku ya afya duniani 7 Aprili 2023, walinda amani wa UN kutoka kikosi cha Tanzania cha kutoa msaada wa haraka, TANZQRF katika kwneye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO nchini DRC wametoa huduma za kupima magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa wakazi wa kijiji cha Nzuma mjini Beni, huko Kivu Kaskazini.

Siku ya Afya Duniani: Walinda amani wa UN kutoka TZ nchini DRC waadhimisha kwa vitendo

Afya

Leo ni siku ya afya duniani ujumbe ukiwa ni Afya kwa Wote ambapo walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, wametumia siku hii kuwapima magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs, wakazi wa Beni-Mavivi jimboni Kivu.

Wakati wa siku ya afya duniani 7 Aprili 2023, walinda amani wa UN kutoka kikosi cha Tanzania cha kutoa msaada wa haraka, TANZQRF katika kwneye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO nchini DRC  wametoa huduma za kupima magonjwa yasiyo ya ku…
TANZAQRF3/Methew Makoba
Wakati wa siku ya afya duniani 7 Aprili 2023, walinda amani wa UN kutoka kikosi cha Tanzania cha kutoa msaada wa haraka, TANZQRF katika kwneye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO nchini DRC wametoa huduma za kupima magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa wakazi wa kijiji cha Nzuma mjini Beni, huko Kivu Kaskazini.

Afisa habari wa kikundi hich cha tatu cha kikosi cha Tanzania cha kutoa msaada wa haraka, TANZ-QRF-3 ndani ya MONUSCO, Luteni Abubakar Muna ndiye alikuwa shuhuda wetu wa tukio hilo la leo ambapo amezungumza na Mganga Mkuu wa TANZ -QRF -3 Luteni Hussen Sinda.

Luteni Sinda anasema, “Tumeona tuadhimishe siku hii kwa kuwapima afya ndugu zetu wa Nzuma na kuwashauri kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari na saratani mbalimbali. Magonjwa haya hayaambukizi kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine, lakini ni magonjwa tunayapata kulingana na namna tunavyoishi maisha yetu.”

Tunawashukuru waliobuni siku hii

Jusue Kapisa ambaye ni Chifu wa Kata ya Nzuma eneo la Beni-Mavivi anasema ushirikiano kati ya walinda amani wa UN kutoka Tanzania na eneo lao umekuwa ni mzuri tangu kuanza kuweko kwa walinda amani hao.

Na zaidi ya yote, tunashukuru viongozi wa afya ulimwenguni kwa kuwazia na kupanga siku ya leo ya kuzungumzia siku ya afya. Sasa hawa viongozi wa afya duniani waone jinsi ya kuendelea kufanya utafiti ili magonjwa yaliyoko duniani na hayana tiba, yapate tiba na wakazi wa dunia waone mambo ya afya yanasonga mbele.”

Upatikanaji wa dawa ni shida, waasi wanatukwamisha

Alphonsine Muhindi, mkazi wa kata ya Nzuma ameshiriki pia huduma hii ya kupima afya na baada ya kupata huduma hiyo anafunguka kuhusu changamoto akisema, “tunapitia shida ya afya hapa Nzuma kwa sababu kwenye afya hatuna dawa kwa kuwa hatuna fedha. Ukisema ulime ili upate fedha, sasa ukiwa shambani unasikia waasi wamefika shambani. Hii inaleta dhiki kwa jamaa kwanza, njaa na magonjwa yanazidi kusambaa kwa kuwa hatuna dawa.”

Tweet URL

Ameshukuru kuweko kwa huduma hii kwa sababu angalau akishapima atajua hali ya afya yao inakuwa ni rahisi kwenda kupata dawa kwani tayari wanafahamu hali yao ya afya na pia kushughulikia watoto.

Hoja ya wananchi yajibiwa na TANZ-QRF-3

Kwa Luteni Martha Mapunda, mtaalamu wa masuala ya saikolojia ndani ya TANZ -QRF -3 ombi lake ni kwa MONUSCO kuongeza idadi ya maafisa wa Jinsia zote wenye taaluma ya saikolojia ili waweze kuwasaidia wakazi wa Beni jimboni Kivu kaskazini.

Hoja ya uhaba wa dawa unaokabili wakazi wa kata ya Nzuma ikajibiwa na Kapteni Damasi Khaza, Afisa Uhusiano wa TANZ-QRF -3 kwa niaba ya kamanda kikosi Luteni Kanali Adson Mwashifungwe ambapo amesema, utaratibu wa ugawaji dawa utafanyika kwa kuzipeleka kwenye vituo vya afya na hospitali ili zipatiwe wakazi hao.

Taarifa hii imeandaliwa kwa pamoja na Luteni Abubakar Muna Afisa Habari TANZ-QRF -3 na George Musubao wa UN News.