Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa jeshi la wananchi la Tanzania watembelea vikosi vya FIB nchini DRC

Ujumbe wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) watembelea vikosi vya FIB MONUSCO nchini DRC.
Abubakar Muna/JWTZ
Ujumbe wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) watembelea vikosi vya FIB MONUSCO nchini DRC.

Ujumbe wa jeshi la wananchi la Tanzania watembelea vikosi vya FIB nchini DRC

Amani na Usalama

Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Brigedia Jenerali Geoge Mwita Itang’are akiwa ameambatana na ujumbe wake kutoka makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania (JWTZ) kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya ulinzi ya Tanzania Jenerali John Jacob Mkunda umefanya ziara ya kutembelea makao makuu ya majeshi ya Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  DRC ujulikanao kama MONUSCO kwenye eneo la Goma na kukutana na kamanda wa vikosi hivyo Luteni Jenerali Otavio Rodrigues De Miranda Filho.

Baadaye ujumbe huo ulielekea mjini Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini yalipo Makao Mako ya vikosi vya kujibu mashambulizi vya FIB vilivyo chini  MONUSCO na kukutana na na kuzungumza na uongozi wa FIB.

Ukiwa Beni ujumbe huo ulibisha hodi katika eneo la Mavivi  ambako ndiko yalipo makao makuu ya vikosi kutoka Tanzania vinavyohudumu katika operesheni za ulinzi wa amani nchini DRC , hapo uugeni huo ulipokelewa na mwenyeji wake kamanda wa kikosi cha 10 cha Tanzania TANZBATT-10 Luteni kanali John Peter Kalabaka.

Ujumbe wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) watembelea vikosi vya FIB MONUSCO nchini DRC.
Abubakar Muna/JWTZ

Kazi inayofanywa na vikosi vya Tanzania

Dhumuni la ziara hiyo ni kutembelea vikosi mbalimbali kutoka Tanzania vinavyohudumu katika operesheni za ulinzi wa amani nchini DRC na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na vikundi hivyo  ikiwa ni Pamoja na kulinda raia wa Congo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali ya DRC na  mamlaka za kiraia ili kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana  nchini DRC.

Brigedia Jenerali Itanga’re akiwa kwenye makao makuu ya vikosi kutoka Tanzania (TAC HQ) Mavivi jimboni Kivu Kaskazini pia amekutana na maafisa na askari katika kikao kifupi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kilimanjaro kwa lengo la kusisitiza mambo kadhaa huku akitilia mkazo maswala ya kinidhamu kwa ujumla , Kuwapongeza maafisa na askari kwa utendaji   kazi mzuri na  weledi,  katika kutekeleza majukumu ya ulinzi wa amani na kuendelea kushurikiana na vyombo vya ulinzi na usalama  vya serikali ya DRC ukizingatia Tanzania na nchi ya DRC ni ndugu na tumekuwa na mahusiano mazuri .

Ujumbe wa Jeshi la Wananchi la Tanzania, JWTZ watembelea vikosi vya FIB MONUSCO nchini DRC.
Abubakar Muna/JWTZ

Pia katika ziara hiyo ujumbe huo wa Tanzania umekutana na meya wa mji wa Beni Jenerali Muteba Kashale Narcisse na kuzungumza na maafisa wa FIB kutoka             Tanzania.

Katika mkutano wao Meja Jenerali Muteba Kashale Narcisse ametoa pongezi za dhati kwa mkuu wa majeshi ya ulinzi ya wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda na kusema kuwa Wananchi wa Tanzania na Congo ni ndugu wamoja na wote ni Waafrika tuko taifa moja”.

Vilevile Jenerali Narcisse amesisitiza kuwa “upendo ambao tunao sisi Waafrika ni upendo wa nguvu na wakiroho hivyo maafisa na askari wote kutoka Tanzania wanaohudumu katika ulinzi wa amani DRC chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa MONUSCO ni ndugu zetu”.

Mwisho Meya huyo ameishukuru Tanzania kwa kutoa wanajeshi wake kuja nchini DRC kusaidia katika harakati za kupatikana kwa amani ya kudumu.