Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nilitekwa nyara na waasi, lakini MONUSCO ilinikomboa- Mwananchi DRC 

Prime Metal, mnufaika wa mradi wa RAPID IMPACT PROJECT nchini DRC ambaye aliwahi kutekwa nyara na kuokolewa juhudi za MONUSCO .
Byobe Malenga/UN News
Prime Metal, mnufaika wa mradi wa RAPID IMPACT PROJECT nchini DRC ambaye aliwahi kutekwa nyara na kuokolewa juhudi za MONUSCO .

Nilitekwa nyara na waasi, lakini MONUSCO ilinikomboa- Mwananchi DRC 

Amani na Usalama

Wiki hii dunia imeadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Tangu mwaka huo zaidi ya wafanyakazi milioni mbili waliovalia sare kijeshi na raia wamesaidia nchi kuhama kutoka vita hadi kwenye amani. Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umekuweko tangu mwaka 2000, ikimaanisha mwaka huu ni miaka 23.

Soundcloud

Raia pamoja na asasi za kiraia nchini humo wamepongenza kazi za MONUSCO ijapokuwa bado kuna mengi ya kutekeleza ili kurejesha amani hasa katika eneo la mashariki mwa DRC linalokumbwa na vita kwa miongo kdhaa sasa 

MONUSCO inasaidia wanawake kujikinga na ukatili wa kingono 

Miongoni mwa raia hao ni Adel Mwasimuke mkazi wa Kinshasa, mji mkuu wa DRC ambaye anasema, “kazi ambazo nazitambua za Monusco ya kwanza ni kwa wafanyakazi wa kibinadamu wa MONUSCO. Wanasaidia kurahisisha usafiri kupitia ndege zao. Pili ni mafunzo ya wanawake hasa namna ya kujikinga na vitendo vya ukatili wa kingono na pia maendeleo ya vijijini kama vile kupatia wananchi maji, na pia kusaidia vikundi mbalimbali kwa kuwapatia fedha za kuendesha miradi mbalimbali” 

Mbali na hayo ya Adel, Prime Metal ambaye aliwahi kutekwa nyara na kuokolewa juhudi za MONUSCO anafunguka akisema, “niko miongoni mwa watu walionufaika na MONUSCO maana nilitekwa nyara katika mbuga ya wanyama ya Virunga mwaka 2015. Nilikaa hapo siku tatu. Wateka nyara walikuwa wakiomba kikombozi lakini MONUSCO waliweza kuniokoa kutoka mikononi mwa wahalifu. Pia mimi nilifaidika na mafunzo katika mradi RAPID IMPACT PROJECT. MONUSCO imejenga pia magereza hasa gereza la Butembo ambapo MONUSCO imelipanua kwani awali likuwa na lijaa wafungwa wengi kupita kiasi na pia kwa chakula”. 

Vikundi vya kiraia vinanufaika na miradi kutoka MONUSCO 

Vikosi vya MONUSCO vimekuwa pia vikitekeleza miradi ya maendeleo kwa kusaidia vikundi vya wanawake kwa kuwapatia mafunzo pamoja na kuwapa pesa hasa wahanga wa vitendo vya ubakaji kama anavyosema hapa Magy Banza, “kwenye Monusco kunakuwa na tawi la akina mama na kukinga watoto na kupitia hiyo, MONUSCO  imeweza kusaidia kupatia vikundi vya wanawake fedha za kusaidia wanawake kisheria, na wale waathirika wa vitendo vya ubakaji. MONUSCO imesaidia sana kesi ziweze kukamilika haraka na wanaopatikana na hatia ya ubakaji waliadhibiwa. MONUSCO inasaidia pia kupokonya silaha na kurahisisha kuwarejesha katika maisha ya kawaida waliotumikishwa vitani. Kuna watoto pia wameweza kuondolewa kijeshi kiujumla kazi za MONUSCO ni nyingi sana”. 

Moise Lameck, Mkazi wa Kinshasa anashukuru MONUSCO kwa kusimama na raia nchini DRC na kutetea haki zao za kibinadamu.
Byobe Malenga/UN News
Moise Lameck, Mkazi wa Kinshasa anashukuru MONUSCO kwa kusimama na raia nchini DRC na kutetea haki zao za kibinadamu.

MONUSCO imejizatiti kutekeleza majukumu yake 

Lakini hata hivyo bado vikosi hivyo vya Umoja wa mataifa vinakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi na hata viongozi wa DRC kwa kile wanachodai kwamba vimeshindwa kudhibiti usalama hasa katika eneo la mashariki mwa DRC. Lakini Moise Lameck anasema kuwa MONUSCO imekuwa ikitetea haki yake akisema, “kwanza MONUSCO ilikuwa nzuri sana ilipokuja matumaini yetu yalikuwa kwa MONUSCO na ilifanya kazi kweli huku wengine hawataki ukweli wa MONUSCO na hiyo ndio shida. Uwepo wake ni mzuri sana”. 

 

Taarifa hii imeandaliwa na  Byobe Malenga, Mwandishi wa Habari wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Kinshasa, DRC.