Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Makala Maalum

Mabadiliko ya tabianchi yanachangia hali ya ukame katika maeneo mbalimbali duniani.
© WMO/Fouad Abdeladim

UDADAVUZI: COP28 ni nini, na kwa nini ni muhimu?

Hali ya joto duniani inaendelea kufikia viwango vya juu na kuvunja rekodi na, mwaka unavyofikia ukingoni, joto la kidiplomasia linaongezeka huku macho yote yakielekezwa Dubai, Falme za Kiarabu, ambako viongozi wa dunia wanakutana kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba, ili kutathmini njia za kusonga mbele katika vita vya dunia dhidi ya mabadiliko tabianchi.

Didas Byaruhanga, mwenye umri wa miaka 64 anayeishi na VVU na kisukari nchini Uganda.
WHO

Kisukari ni moja ya muuaji mkubwa kwa wenye VVU Uganda: WHO

Jijini Kampala, nchini Uganda, zaidi ya watu milioni 1.4 wanaishi na virusi vya ukimwi  VVU na kati ya hao, asilimia 5.8 wana ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa wa kisukari ni kawaida miongoni mwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na ni mojawapo ya sababu kuu za vifo miongoni mwa watu hao kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO.