Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiwewe, msongo wa mawazo na simanzi vimekita miziz Gaza: UNICEF Elder

Msichana akipumzika katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Gaza.
© UNICEF/Abed Zaqout
Msichana akipumzika katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Gaza.

Kiwewe, msongo wa mawazo na simanzi vimekita miziz Gaza: UNICEF Elder

Amani na Usalama

Ukiwatazama watu  huko Gaza nyuzo zao zinaonyesha "kiwewe, msongo wa mawazo, huzuni na simazi vikiwa vimekita mizizi ", kwa mujibu wa James Elder, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF ambaye amejiunga na juhudi za kufikisha misaada ya kibinadamu katika eneo lililozingirwa. 

Bwana Elder amekutana na watoto na familia zao huko Gaza, wakati huu sagini usitishwaji uhasama kwa minajili ya kibinadamu mapigano, ambayo yamesita baada ya wiki za mashambulizi makali ya makombora na mabomu yaliyoua na kujeruhi maelfu na kuwatawanya Wapalestina milioni 1.7.

Mzozo huo ulianza tarehe 7 Oktoba, wakati Hamas iliposhambulia Israel, na kuua zaidi ya watu 1,200 na kuwakamata mateka zaidi ya 200.

"Hali katika eneo hili inaonekana ya kukata tamaa, iwe ni muundo halisi au kuona tu ghorofa baada ya jengo linguine la ghorofa kuporomoka, vifusi vilivyoharibiwa chini, saruji, magari yaliyolipuliwa, watu wanaokimbia nyumba zao, au ikiwa ni taswira tu ya nyuso za watu, kiwewe, msongo wa mawazo, kana kwamba huzuni na hsimanzi vimekita mizizi hapa Gaza.”

Ameongeza kuwa ni wakati mgumu sana hivi sasa, na, bila shaka, hii ni kweli kwamba usitishaji uhasama kwa minajili ya kibinadamu watu wanapata nafuu kutokana na mambo mengi waliyoyapitia katika wiki saba zilizopita na wanahofia sana kwamba mambo yataanza tena.

Lakini, watu milioni 1.5 wamepoteza makazi yao, watu wako katika makazi mbalimbali, hospitali zimejaa watoto wenye majeraha ya vita.

Ukweli wa kutisha

Ameongeza kuwa “Inatisha. Kila mtoto hapa, naweza kusema kwamba kwa uhakika wote watahitaji aina fulani ya msaada wa kisaikolojia. Kijana mdogo niliyekuwa nazungumza naye nusu saa iliyopita katika kile kinachopaswa kuwa chuo cha ufundi cha vijana lakini sasa ni kambi ya watu 30,000 au 40,000, amepoteza mama yake, amepoteza dada zake kwa bomu. Bado hajui kuwa mama yake alikufa.”

Huu ndio ukweli wenyewe. Nimezungumza na familia nyingi sana, na bado hawajamwambia mtoto ambaye bado anapona kutokana na majeraha ya vita kwamba mtu mwingine ambaye wanampenda pia amekufa, kwamba maisha yao kwa kweli ni mabaya zaidi kuliko walivyofikiria.

Uwanja wa vita

Kwa mujibu wa bwana Elder hospitali zimejaa. Kuna wodi za dharura zilizofurika wavulana na wasichana wenye majeraha ya mabaya ya moto wa kutisha.

Hawako tu kwenye vitanda vya hospitali ndani. Wafanyikazi hawa ambao ni wahudumu wa afya wenye ujasiri wa wa ajabu, madaktari wa ajabu, wauguzi wanafanya kazi kutwa kucha sasa wameishiwa nafasi ya kuongeza wagonjwa wengine.

“Ni uwanja vita. Una watoto katika viwanja vya magari na bustani, kwenye vitanda kila mahali. Kisha, bila shaka, kuna mamia ya maelfu ya watoto ambao hawako shuleni, walio katika kambi zilizojaa sana, ambako ni baridi, hawana chakula cha kutosha, hawana maji ya kutosha, ambao sasa wako hatarini kwa mlipuko wa magonjwa. Ni hali ya kutisha.”

Kwa bahati mbaya, kila ninapogeuka, mtu ana hadithi nyingine ambayo inaweza kuvunja moyo wangu tena sasa hivi katika saa ya mwisho. Wote wanabaki kichwani mwangu haswa wale ambao wameteseka sana kupitia mapigano.

Barabara huko Gaza tarehe 8 Oktoba 2023. (Maktaba)
© UNRWA/Mohammed Hinnawi
Barabara huko Gaza tarehe 8 Oktoba 2023. (Maktaba)

Miili iliyoharibika

Nilikuwa kwenye basi na watoto. Ilikuwa imechukua siku nne kutoka hospitali za kaskazini. Mvulana huyu mdogo alikuwa kwenye basi kwa siku nyingi, huku sehemu ya chini ya mguu wake ikiwa imekatwa. Siku nne kwa mwili wake kuanza kuoza, na viungo vilivyovunjika.

Ni zaidi ya kiwango chochote cha kuelewa jinsi hali hii ilivyotokea kwa kiwango kama hicho, na kwa hivyo, moja ya sababu ambazo tunaendelea kuzungumza sana ni kwamba hali hii haiwezi kuendelea.

Mvulana mdogo, Omar, alikuwa na umri wa miaka saba wakati nyumba ya familia yake iliposambaratishwa kwa kombora. Mama yake aliuawa, baba yake aliuawa na ndugu pacha wa Omar aliuawa. 

Hata nilipozungumza naye, aliweza kushiriki tu kile anachofanya. Anampenda shangazi yake. Ni mtu mzuri sana na anamsidia.

Lakini, aliendelea kufumba macho, na nilikuwa nikijaribu kuelewa kwa nini. Nilimuuliza shangazi kwa nini, na akasema anaogopa sana kwamba atasahau jinsi mama yake na baba yake wanavyofanana. Hii ndio hofu yake sasa. Na kwa hiyo, anafunga macho yake kwa sababu hawezi kuvumilia mawazo kwamba amewapoteza katika ulimwengu huu, lakini pia anaweza kuwapoteza katika mawazo yake.

Kufuatia mlipuko, Sondos, mama mwenye umri wa miaka 26 alipasuliwa kwa dharura, akimtaja mtoto wake mchanga Habiba kwa kumbukumbu ya bintiye mwingine aliyeuawa siku hiyo hiyo.
© UNFPA/Bisan Ouda
Kufuatia mlipuko, Sondos, mama mwenye umri wa miaka 26 alipasuliwa kwa dharura, akimtaja mtoto wake mchanga Habiba kwa kumbukumbu ya bintiye mwingine aliyeuawa siku hiyo hiyo.

Usitishaji mapigano umeleta ahueni

Siku chache zilizopita, mashirika yote ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakifanya kila yawezalo. 

Shirika la kuhudumia watoto UNICEF limeleta vifaa vya matibabu, vifaa vya dharura kwa ajili ya wakunga kwa sababu kulikuwa na wanawake wengi wajawazito wanaojifungua katika eneo la vita, chumvi ya kunyweshwa ya kurejesha maji mwilini, suluhisho la mishipa na multivitamini kwa watoto kwa sababu tuna wasiwasi sana kuhusu hali yao ya lishe.

Shirika la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNWRA, shirika kubwa zaidi hapa kwa ajili ya watu wa Ukanda wa Gaza, linatoa chakula, mafuta na maji. Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP linasambaza chakula, na dawa zinasambazwa na Shirika la Afya Duniani WHO.

Watu wanahitaji muda ili kupona

Usitishaji huu wa mapigano kwa ajili ya masuala ya kibinadamu ni lazima, kwa dhamira njema, ugeuke kuwa usitishaji mapigano wa kibinadamu na kisha amani ya kudumu.

Zaidi ya wavulana na wasichana 6,000 wameuawa. Hali hiyo lazima ikome. Watoto wengi sana wamepoteza wazazi, wazazi wengi wamepoteza watoto.

Nimekuwa hapa tu tangu wiki iliyopita. Si kawaida sana kuzungumza na mtu yeyote hapa ambaye hajapoteza mpendwa wake.

Hatuwezi kutoka katika hali ya kupata msaada huu ndani ya saa 24 au 72 na kurejea tena kwenye mashambulizi.

Watu wanahitaji muda wa kupona na tunahitaji muda wa kutoa misaada. Ndio maana amani ya kudumu ndio kitu pekee ambacho hatimaye kitawalinda watu hapa.

Wavulana wawili wakibeba chupa za maji katika kambi ya wakimbizi inayofadhiliwa na UNWRA huko Khan Younis kusini mwa Gaza.
© UNICEF/Abed Zaqout
Wavulana wawili wakibeba chupa za maji katika kambi ya wakimbizi inayofadhiliwa na UNWRA huko Khan Younis kusini mwa Gaza.

Maji ni tofauti kati ya uhai na kifo

Maji yatakuwa ni tofauti kati ya uhai na kifo. UNICEF na washirika wetu wote wa  hapa Ukanda wa Gaza wana mpango wazi kabisa.

Tunahitaji amani. Mabomu yanapaswa kukoma kwa sababu yanaharibu mitambo ya kuondoa chumvi ambayo ni muhimu hapa.

Tunahitaji kupata mafuta ndani ya Gaza tufanye matengenezo. Tunahitaji mashine kurekebisha mitambo na mabomba yafunguliwe tena.

Bila shaka, tunaweza kusambaza mamia ya maelfu ya chupa za maji, lakini sio njia bora ya kutoa misaada, na haitawafikia watu haraka vya kutosha.