Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MAHOJIANO: Maazimio ya Baraza kuu yanawakilisha dhamira ya ubinadamu: Dennis Francis

Rais wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la UN Balozi Dennis Francis akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa New York Marekani Novemba 2023
UN Video
Rais wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la UN Balozi Dennis Francis akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa New York Marekani Novemba 2023

MAHOJIANO: Maazimio ya Baraza kuu yanawakilisha dhamira ya ubinadamu: Dennis Francis

Amani na Usalama

Azimio la hivi karibuni kabisa la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linalotaka kuwepo na usitishwaji wa uhasa Gaza kwa nminajili ya kibinadamu ni mfano mmoja tu wa jinsi gani chombo hicho cha Umoja wa Mataifa chenye wanachama 193 kinavyotanabaisha dhamira ya kimataifa.

 

Rais wa Baraza Kuu laUN Balozi Dennis Francis akifunga mjadala mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la UN tarehe 26 Septemba 2023
UN /Cia Pak
Rais wa Baraza Kuu laUN Balozi Dennis Francis akifunga mjadala mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la UN tarehe 26 Septemba 2023

Akihojiwa na UN News Rais wa Baraza Kuu Denis Francis amesema “Huwa hatupati kupitishwa kwa kaulimoja kwa maazimio lakini ulinapoungwa mkono na theluthi mbili ya kura, hiyo ni ishara yenye nguvu , na ujumbe mzito wa makubaliano, na umoja.”

Haki sawa ya kupiga kura

Francis amesema kama chombo kikuu cha kutunga será cha Umoja wa Mataifa Baraza Kuu ndipo mahali ambapo nchi zote wanchama wana haki sawa ya kupiga kura ya masuala mbalimbali yaliyo mnele yao, ikiwemo masuala ya amani na usalama.

Ingawa maazimio yake hayawajibishi lakini “Yanatoa azimio la kisiasa kama sehemu ya wajumbe waliowengi wa jumuiya ya kimataifa.” Bwana Francis ameshika wadhifa huo kama Rais wa Baraza Kuu mwezi Septemba na ataongoza chombo hicho kwa muda wa mwaka mmoja.

Tangu wakati huo, amekuwa akiongoza mikutano juu ya mada ambazo ni pamoja na kuokoa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), kujiandaa kwa janga lijalo la kimataifa, kuhakikisha huduma za afya kwa watu wote na kuleta mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mwanadiplomasia huyo mkongwe kutoka Trinidad na Tobago hivi majuzi aliketi na UN News kutafakari juu ya vipaumbele vyake, jukumu muhimu la Baraza Kuu, na kwa nini wakosoaji wanapaswa kushirikiana na Umoja wa Mataifa.

Vipaumbele vya Denis Francis

Mkuu huyo wa Baraza Kuu amesema vipaumbele vyake vimejikita katika masuala manne ambayo ni Amani, ustawi, maendeleo na uendelevu.

Amesema mambo haya yote ni muhimu sana na mara nyingi huingiliana  Je anahakikisha vipi nchi zinaungana kuyashughulijia?

“Ni kweli yana muingiliano  na hasa kupitia ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu SDGs kwa sababu hiyo ndio jenda ya maendeleo inayounganisha wote na kuzileta nchi zote 193 kuchukua hatua kwa makubaliano ya pamoja kuwatoa watu katika umasikini , kunyimwa haki, utapiamlo, njaa na kujenga mazingira ya kubadilisha Ulimwengu na kuwa katika mfumo endelevu na wenye ufanisi, hivyo ni kwa ajili ya sayari kama ilivyo kwa watu.”

Ameongeza kuwa lakini pia lakini pia tumeunganishwa kwa njia nyingine kwa sababu wakati amani na usalama vinavurugika, kama vile ambavyo imekuwa katika miaka miwili au mitatu iliyopita haswa, athari zake ni kwa kila mtu.

“Ni kwa nia yetu sote kuchagiza na kudumisha amani kwa sababu ukosefu wa amani, ukosefu wa maelewano katika mfumo, hudhoofisha mfumo na kufanya kuwa magumu sana malengo mengine yote makubwa tuliyo nayo

Dennis Francis (Katikati) Rais wa kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati wa uwasilishwaji wa Ajenda ya Pamoja
UN Photo/Paulo Filgueiras
Dennis Francis (Katikati) Rais wa kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati wa uwasilishwaji wa Ajenda ya Pamoja

 

Je Baraza Kuu lina ushawishi wowote kusitisha kinachoendelea Mashariki ya Kati?

Rais huyo wa Baraza Kuu amejibu kwamba “Kweli, tunao kwa sababu wiki mbili na nusu zilizopita Baraza Kuu lilipitisha kwa mafanikio azimio la kwanza kutoka kwa mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Gaza, likitaka kusitishwa kwa mapigano, kuachiliwa huru bila masharti kwa mateka wote. na kuhakikisha utoaji wa misaada na usaidizi wa kibinadamu.”

Sasa, kwa kuzingatia ukweli kwamba wakati huo, Baraza la Usalama lilikuwa limekutana na kujaribu kukubaliana azimio mara nne tofauti na limeshindwa. Kwa hiyo, Baraza Kuu kwa kweli liliweza kutoa azimio ambalo kulikuwa na maafikiano makubwa nchi 121, naamini, ziliunga mkono.

Hilo nadhani limekuwa mchango mkubwa sana uliotolewa na Umoja wa Mataifa kwa sababu katika kuendeleza malengo ya mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambayo ni kuwaokoa binadamu na janga la vita, tuliweza kuleta azimio hili kama njia ya kusitisha vita. 

Tumesema waziwazi katika azimio hilo kwamba kile ambacho Baraza Kuu linahitaji, na kutamani ni usitishaji mapigano ili kuokoa maisha ya binadamu, watu 11,000 waliokufa kutokana na hatua dhidi ya Gaza ni wengi mno. Haisemeki na haikubaliki. 

Na kwa hivyo, tumetoa wito kwa hilo, lakini pia tukitilia mkazo ulazima wa Hamas kuwarudisha mateka kwa familia zao bila masharti.

Ingawa maazimio ya Baraza Kuu hayawajibishi , je yana uzito wa kimaadili?

Bwana Francis amesema “Kabisa. Yanatoa tamko la kisiasa kwa upande wa wanachama wengi wa jumuiya ya kimataifa. Na kwa maana fulani, wanaunda aina ya sheria laini kwa sababu maazimio ya Baraza Kuu yanawakilisha, kwa maana fulani, dhamiri ya ubinadamu, mtazamo mkuu wa ubinadamu.

Kamwe hatupati umoja katika maazimio lakini unapoweza kuamuru zaidi ya theluthi mbili ya kura ndani ya Baraza, hiyo ni ishara yenye nguvu, ujumbe wenye nguvu, wa makubaliano. Na ndivyo tulivyoweza kufanya. Wito wetu kwa wahusika wote ni kwamba wangeheshimu na kutekeleza azimio hilo pamoja na azimio lililokubaliwa Jumatano katika Baraza la Usalama.

Baraza Kuu likipitisha azimio kuhusu ulinzi wa Rais Gaza a utekelezaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu (Kutoka Maktaba)
UN Photo/Evan Schneider
Baraza Kuu likipitisha azimio kuhusu ulinzi wa Rais Gaza a utekelezaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu (Kutoka Maktaba)

Unapozungumzia kuwa hili ni onyesho la dhamiri ya Mataifa mengi Wanachama wa Umoja wa Mataifa lakini je, hiyo inatosha? 

Dennis Francis amesema  Lakini wazo ni muhimu! Ukisikiliza kwa makini misimamo na maoni yanayoakisiwa, mjadala mkubwa ni kuhusu kanuni na maadili, kwa hivyo mawazo hayana maana. Siasa huibuka tu kwani kuna maoni tofauti na kukinzana, kwa hivyo mawazo huhesabiwa kuwa yana nguvu.

Ndiyo maana azimio lililopitishwa katika Baraza Kuu lina umuhimu wa hali ya juu kwa sababu lina ujumbe mzito wa kisiasa. Ndiyo maana nchi hujadili maazimio haya kwa nguvu na ari kama hiyo kwa sababu wanathamini athari yanayoweza kuwa nayo hadharani.

Nchi nyingi ninazozifahamu haziko vizuri hujihisi zimetengwa kisiasa. Nchi ni kama binadamu. Wanadamu wanapenda kuthaminiwa, kupendwa, wanapenda kujisikia heshima na kuungwa mkono na marafiki zao, wanataka kujihusisha, wanataka kufanya mazungumzo. Tulikusudiwa kuwa hivyo.

Nchi sio tofauti kwa sababu unapojenga madaraja hayo ya mahusiano, inaongeza nafasi ambayo unaweza kutenda kama nchi, kama mtu huru. Wakati huna mahusiano hayo yanayosaidia, unakuwa na machaguo finyu sana.

Na kwa hivyo huo ndio wito wa azimio la Baraza Kuu. Linatoa ujumbe ambao unaweza kuleta mabadiliko makubwa kisiasa. Na kwa kuwa maoni ya umma huwa na jukumu katika mambo haya, lazima tukumbuke hilo.

Kuhusu mzigo wa madeni katika nchi zinazoendelea Baraza Kuu linaweza kufanya nini

Dennis Francis amesema kwa hakika, usanifu wa fedha duniani umepitwa na wakati. Ulianzishwa wakati wa mwishoni mwa miaka ya 1940 ambapo nchi nyingi zilizopo sasa hazikuwepo kabisa. Kinachojulikana kama Global South, Kundi la 77 na China ambalo naamini linajumuisha takriban nchi 140, hazikuwepo.

Kwa hivyo, kuna usanifu wa kifedha wa kimataifa ambao uliundwa kwa wakati tofauti na malengo ambayo hayakuzingatia mahitaji ya maendeleo na vipaumbele au upekee wa nchi zinazoendelea.

Chukua kwa mfano, nchi zisizo na bandari ambazo zinakabiliwa na ugumu mkubwa. Gharama ya kila kitu katika nchi isiyo na bahari kwa wastani ni juu mara mbili ya kuliko ilivyo katika nchi za pwani kwa sababu wametengwa na bahari. Wateja wanaoishi katika nchi hizo wanapaswa kulipa mara mbili ya kile ambacho mtumiaji wa kawaida katika nchi ya pwani atalipa. 

Hiyo ni ugumu. Ni jambo lile lile katika nchi zinazoendelea za Visiwa Vidogo (SIDS), ambazo nyingi zimetengwa kwa sababu ziko mbali na masoko ya kimataifa.

Nimelipa kipaumbele kundi hili la kile tunachorejelea kuwa nchi zilizo katika mazingira hatarishi kwa sababu zimesonga mbele kimaendeleo.

Mfumo huo haujakidhi mahitaji au haujaundwa ili kuzingatia mahitaji ya nchi hizo na kuzisaidia ili kupanda ngazi ya kimaendeleo kwa njia endelevu.

Nchi nyingi za visiwa vidogo zinazoendelea ziko katika tishio kubwa la kupanda kwa kina cha bahari
@UN
Nchi nyingi za visiwa vidogo zinazoendelea ziko katika tishio kubwa la kupanda kwa kina cha bahari

Madai kwamba UN imepitwa na wakati na haina ufanisi ikiwemo Baraza Kuu unayachukuliaje?

Rais huyo wa Baraza Kuu amesema cha kwanza kabisa, watu wana haki ya maoni yao. Ningewahimiza, hata hivyo, wajihusishe nasi zaidi kidogo kwa sababu kile ambacho watu wanaona katika taarifa ya habari kwa dakika moja hakijumuishi kazi nzima ya Umoja wa Mataifa.

Baada ya kusema hayo, ningesema pia kwamba Umoja wa Mataifa wenyewe haujali ukweli kwamba kuna aina ya madai huko nje ya kutoridhishwa na kukatishwa tamaa na jinsi ambavyo umekuwa ukifanya kazi hivi karibuni.

Lakini wacha niseme hivi “Umoja wa Mataifa haupo peke yake. Unaundwa na serikali huru 193. Neno hilo huru ni muhimu sana kwa sababu lina maana kwamba serikali hizo zinaweza na zinafanya maamuzi kwa kuzingatia maslahi na vipaumbele vyao vya kitaifa.”

Umoja wa Mataifa unachokifanya ni kuunda jukwaa la wao kuja pamoja ili kujaribu kukubaliana mbinu za pamoja za matatizo mbalimbali ya kimataifa.

Kwa hivyo, nitauliza hivi “Ikiwa Umoja wa Mataifa hauna umuhimu, ungebadilishwa na nini? Na kwa hivyo, nawaambia watu, asante Mungu Umoja wa Mataifa uko kwa sababu unaunda jukwaa linalohitajika sana la uratibu, mashauriano na ushirikiano kati ya mataifa 193 ambayo yasingekuwa na njia na nafasi ya kukutana, kuratibu, kutatua shida za ulimwengu na masuala menine.”

Hayo ni mafanikio yenye nguvu na yanayoweza kuleta mabadiliko, ya kutisha ambayo Umoja wa Mataifa umeyafanya kwa miaka mingi na, zaidi ya hayo, kuzuia vita ya tatu ya dunia.