Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashine mpya ya kusagisha unga ya UNFPA yawa chachu ya amani kwa wanawake Blue Nile Sudan

Jamii za kijiji cha Shanisha katika Jimbo la Blue Nile nchini Sudan wakisherehekea uwekaji wa kiwanda kipya cha kijiji cha kusagisha unga.
© UNFPA Sudan
Jamii za kijiji cha Shanisha katika Jimbo la Blue Nile nchini Sudan wakisherehekea uwekaji wa kiwanda kipya cha kijiji cha kusagisha unga.

Mashine mpya ya kusagisha unga ya UNFPA yawa chachu ya amani kwa wanawake Blue Nile Sudan

Msaada wa Kibinadamu

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA nchini Sudan Mohamed Lemine, amesema shirika hilo limeweka mashine mpya ya kusagisha unga kwa wanakijiji wa Shanisha, katika jimbo la Blue Nile, nchini Sudan ili kuwapunguzia adha wananchi wa eneo hilo.

Miongoni mwa wanufaika ni Haleema Ibrahim mwenye umri wa mika 36, ambaye alitembea dakika chache kurudi nyumbani kwake katika kijiji cha Shanisha, katika jimbo la Blue Nile nchini Sudan, akiwa amebeba kikapu cha nafaka zilizosagwa kutoka kwenye machine hiyo mpya ya  kusagisha unga. 

Bi. Haleema Ibrahim akiwa amejawa na furaha tele ameliambia shirika la UNFPA, kwamba, “tulikuwa tukitembea umbali mrefu kwenda kusaga nafaka zetu. Wanawake na wasichana walikumbana na unyanyasaji njiani, na ilitubidi kukimbia haraka ili kuukwepa, mara nyingi tukimwaga unga mwingi njiani.” 

Lemine ameendelea kusema kuwa, kama vijiji vingi, Kijiji chake hakijaunganishwa vyema na huduma za msingi za umma, na mara nyingi huwa ni kwa wanawake na watoto hulazimika kutembea umbali wa maili kadhaa kufikia mashine ya kusaga unga, pampu za maji na mambo mengine muhimu. 

Kwa Salma mwenye umri wa miaka 36, ambaye alifika Shanisha kukwepa mzozo uliokuwa ukiendelea katika jiji aliozaliwa huko Khartoum, eneo la mbali amezungumzia masuala yake ya usalama akisema  "Niliandamana na binti yangu kusaga nafaka. Ni safari ya kuchosha. Hakukuwa na mashine ya kusagia katika kijiji chetu, kwa hiyo tulilazimika kusafiri hadi mji wa mbali, ambako watu walitunyanyasa na kutufanyia ukatili njiani”. 

Mwanamke akirudi kutoka kwa kinu kipya cha unga kilichojengwa huko Shanisha, Jimbo la Blue Nile. Wanawake na wasichana nchini Sudan wanakabiliwa na vitisho vya mara kwa mara vya unyanyasaji na mashashambulizi wanaposafiri umbali mrefu, mara nyingi peke y…
© UNFPA Sudan
Mwanamke akirudi kutoka kwa kinu kipya cha unga kilichojengwa huko Shanisha, Jimbo la Blue Nile. Wanawake na wasichana nchini Sudan wanakabiliwa na vitisho vya mara kwa mara vya unyanyasaji na mashashambulizi wanaposafiri umbali mrefu, mara nyingi peke yao, kufikia huduma muhimu.

Wanawake na wasichana wahanga wakubwa wa vita

Zaidi ya hayo, Bwana Lemine, amesema wanawake na wasichana nchini Sudan wanabeba mzigo mkubwa wa athari za vita.

Akiongeza kuwa “Safari za kwenda kwenye maeneo yanayotarajiwa ni ngumu, akina mama wanaobeba watoto migongoni mwao, wanakabiliana na vurugu, shuruti, umaskini, na njaa.”

Katika maeneo mengi UNFPA inasema waliokimbia makazi yao wanajikuta wakishiriki mapambano sawa na wenyeji wao.

Pia chakula na maji safi ni haba, upatikanaji wa huduma za afya ni kama haupo, na mivutano inaongezeka. Unyanyasaji wa kijinsia, ukatili,ukandamizaji, na unyonyaji vimeenea, ambapo mapigano yanaendelea hata katika jamii ambazo watu waliohamishwa wanafika kutafuta usalama.

Aidha, Lemine ameeleza kuwa kadri hali ya uchumi na usalama inavyozidi kuwa mbaya, upatikanaji wa msaada wa afya na ulinzi unazidi kuzorota.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu milioni 4.2 kote nchini Sudan wako katika hatari ya kukabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia huku mzozo huo ukiendelea na upatikanaji wa msaada wa afya na ulinzi unaporomoka.

Mashine hii ni mkombozi kwetu 

Om Kolthom, mwanamke mwenye umri wa miaka 40 kutoka Khartoum ameongeza kuwa "Nilikuwa nikienda kwenye mashine ya kusaga unga na nilikuwa na matatizo mengi. Wakati fulani nilikutana na wanaume sita ambao walidai niwalipe pesa ili niweze kupita." 

Badala ya kujali ustawi wao baada ya kurudi kutoka safari ya kusaga unga wanawake wanasema mara nyingi walikabiliwa na uchunguzi na ukosoaji kutoka kwa wanafamilia. "Wanauliza maswali kama nini kimefanyaa umekaa huko muda mrefu?' na 'Kwa nini umepoteza nusu ya unga?'” Bi Ibrahim alimwambia mwakilishi wa UNFPA.

Bwana Lemine amesema tishio la unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na wasichana nchini Sudan limeenea hadi kufikia hali ya kawaida. 

Wakizungumza na mtandao wa ulinzi wa jamii unaoungwa mkono na UNFPA, unataka kupunguza changamoto hii ya unyanyasaji, kwani watu wengi wameonyesha hitaji la huduma za msingi za karibu, salama, na zinazoweza kufikiwa zaidi, ikiwa ni pamoja na viwanda vya kusaga, ili waweze kulisha familia zao na kulinda uhuru wao wa kimwili. 

Wanawake kutoka jamii za Shanisha wakizungumza na UNFPA kuhusu masuala ya ulinzi yanayowakabili kila siku.
© UNFPA Sudan
Wanawake kutoka jamii za Shanisha wakizungumza na UNFPA kuhusu masuala ya ulinzi yanayowakabili kila siku.

UNFPA imeitikia wito

Wito huo umezingatiwa na UNFP ambayo ikaamua kuleta kinu hicho cha kusaga. Hicho ni kinu cha kwanza kusakinishwa na UNFPA nchini Sudan na hadi sasa kinahudumia takriban watu 30,000 huko Shanisha.

Mwakilishi wa UNFPA nchini Sudan Mohamed Lemine amesema, "Mradi huu ni mfano wa jinsi wanawake na wasichana wanavyoendesha mchakato wa kupanga mipango yetu." 

UNFPA imefanya miradi mingi kama hiyo katika miktadha mingine ya kibinadamu, kama vile kuhakikisha vifaa vya bafu katika kambi za wakimbizi vinamulikwa vizuri na kusambaza filimbi na tochi lakini pia vifaa vya heshima vikijumuisha chupi na visodo vya hedhi. 

Kwa Om Kolthom, kuingilia kati kwa UNFPA kumekuwa afueni. "Kwa kinu hiki kipya, tunaweza kutuma hata mtoto mdogo kutoka nyumbani kwenda kusaga nafaka. Inachukua chini ya dakika 5 sasa."

Programu inayozingatia watu

Kwa mujibu wa UNFPA pamoja na hatari ya unyanyasaji wa kijinsia pia mara nyingi hudhoofisha uwezo wa wanawake na wasichana kuishi pamoja na afya na haki zao za ngono na uzazi, mipango ya jumla inayoendeshwa na waathirika inaweza kuwa muhimu. 

Shukrani kwa washirika kama vile Muungano wa Ulaya, kote Sudan UNFPA imeanzisha mitandao mitano mipya ya ulinzi wa jamii katika maeneo ya Al Jazirah, Darfur Magharibi, Bahari Nyekundu na Majimbo ya Kaskazini na inasaidia mitandao hai 167 kote nchini. 

Nafasi nyingi salama na kliniki za muda pia zimeanzishwa, zikihudumia wanawake na wasichana kutoka jamii zilizohamishwa na zinazowakaribisha. 

Hizi hutoa usaidizi maalum na kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na vifaa vya baada ya ubakaji, usaidizi wa afya ya ngono na uzazi, huduma za kisaikolojia, na msaada wa huduma zingine za gharama.

Tangu katikati ya mwezi Aprili  mwaka wa 2023,UNFPA inasema  zaidi ya watu milioni 6 wamelazimika kukimbia makazi yao nchini Sudan kutokana na mzozo unaoendelea. 

Kati ya hao, milioni 4.8 wamekuwa wakimbizi wa ndani ya nchi yao, zaidi ya robo tatu yao wakiwa wanawake na wasichana walio katika umri wa kuzaa. 

Shirika hilo limesisitiza kuwa wakati mzozo wa Sudan unavyozidi kuimarika, kuna hitaji la dharura la ufadhili wa ziada na hatua ili kulinda usalama na haki za wanawake na wasichana ambao wako katika hatari ya kudhulumiwa na kunyanyaswa