Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
UN yakusanya msaada, mgonjwa wa kwanza wa COVID-19 akibainika makambi ya Rohingya
Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa leo yametangaza hatua zaidi za msaada na ombi la fedha ili kuzuia kusambaa kwa mlipuko wa ugonjwa wa corona au COVID-19 baada ya mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa kwenye makazi yaliyofurika ya wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh.
15 Mei 2020
Hii leo Ijumaa kama kawaida ni mada kwa kina na tunammulika muuguzi mkunga kutoka hospitali ya Kairuki nchini Tanzania akiangazia ni kwa vipi wanatekeleza majukumu yao ipasavyo katikati ya janga la virusi vya Corona au COVID-19. Muuguzi mkunga huyo amezungumza na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam. Tutajifunza neno la wiki na mtaalamu Onni Sigalla anachambua neno Kiruka Njia. Habari kwa ufupi nazo zimo tukiangazia ndege ya kwanza ya abiria kutua Tanzania kupambana na COVID-19.
Rwanda yapatia MINUSCA mashine ya kupima COVID-19
Kikosi cha Rwanda kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA kimepatia maabara ya kitaifa ya kibayologia nchini humo mashine yenye thamani ya dola 200,000 kwa ajili ya kupima ugonjwa virusi vya Corona au COVID-19.
Nimeongeza uzalishaji sabuni, nikapunguza bei, ili kupambana na COVID-19-Havyarimana
Ili kusaidia kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona, mkimbizi kutoka Burundi, Innocent Havyarimana anayeishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya na ambaye kwa miaka mitano amekuwa akijihusisha na utengenezaji wa sabuni za maji, hivi sasa ameongeza uzalishaji na kupunguza bei ya sabuni ili watu wengi waweze kunawa mikono yao.
Viongozi wa dunia washikamana kwa wito wa fursa ya chanjo kwa wote dhidi ya COVID-19
Zaidi ya viongozi wa kimataifa 150 leo wamezindua wito wa fursa kwa wote ya upatikanaji wa chanjo ya virusi vya corona au COVID-19 katika siku za usoni.
UNMISS yasambaza tenki za maji sokoni kudhibiti COVID-19 Juba Sudan Kusini
Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS, katika kuunga mkono juhudi za kitaifa za kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona au COVID-19, wamesambaza tenki za maji katika maeneo ya soko yenye msongamano wa watu mjini Juba.
14 Mei 2020
Mwakilishi wa WHO Burundi afurushwa, ofisi ya WHO kanda ya Afrika yazungumza. Huko Sudan Kusini UNMISS yaingia sokoni, kulikoni? Katibu Mkuu wa UN azindua sera ya kusaida afya ya akili wakati huu wa janga la Corona au COVID-19, na mashinani tunakwenda Ituri nchini DRC, kilio cha mama mkimbizi wa ndani na makala ni nchini Kenya. Karibu!
Afya ya akili ni msingi wa kila kitu kwenye COVID-19 - Guterres
Ugonjwa wa virusi vya Corona ukiendelea kutikisa dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezindua muhtasari wa mkakati wa kushughulikia afya ya akili ambayo hivi sasa inatetereka kutokana na janga la COVID-19.
Burundi yamfurusha Mkuu wa WHO siku chache kabla ya uchaguzi mkuu, WHO yazungumza
Shirika la afya la Umoja la Umoja wa Mataifa, WHO, limesema linawasiliana na serikali ya Burundi ili kufahamu sababu ya kufukuzwa kwa mwakilishi wake nchini humo pamoja na wafanyakazi wengine watatu. Serikali ya Burundi ilitangaza jana kumfukuza mwakilishi huyo Dkt. Walter Kazadi Mulombo, ikiwa ni siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo.
WFP yaendelea kunusuru wahitaji, katikati ya COVID-19,
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula, WFP, linaendelea kusaka rasilimali ili liweze kufikisha misaada kwa watu milioni 100 kwa mwaka huu 2020. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.
Misaada hiyo ikiwemo ya chakula ni muhimu kwa jamii zilizo hatarini ambapo WFP inasema kuwa kuimarisha mifumo ya hifadhi ya jamii ni muhimu ili watu wengine milioni 130 wasitumbukie kwenye njaa kutokana na janga la virusi vya Corona au COVID-19.