Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

19 Mei 2020

Hii leo tunamulika COVID-19 na athari zake kwa watu wasio na chakula ambapo ripoti inasema umaskini utaua watu zaidi kuliko virusi vyenyewe. Kuelekea siku ya nyuki duniani kesho, tumezungumza na wanahabari wanaofuga nyuki Tanzania. Nchini Kenya madhehebu ya kikatoliki yaunga mkono upanzi wa miti, makala tunatamatishia huko Kakonko mkoani Kigoma na mashinani tunabisha hodi Kenya. Mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Sauti
12'48"
Marafiki wawili wanaounga mkono haki za wapenzi wa jinsia moja wakiwa kwenye maandamano jijini New York, Marekani (2018)
UN News/Elizabeth Scaffidi

COVID-19 yaongeza chumvi katika kidonda cha LGBTI

Hii leo dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, waliobadili jinsia na wale wenye wapenzi wa jinsia zote, IDAHOT, katika changamoto kubwa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii ya leo 17 Mei.