Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Kala Jeremiah anayesifika kwa nyimbo za kijamii, sasa aja na CORONA IPO.
Wakati mapambano dhidi ya virusi vya corona yakiendelea duniani kote, wito umekuwa ukitolewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kuwa ni jukumu la kila mtu kuwalinda wengine kama anavyojilinda hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaza elimu ya kutosha kwa jamii kuhusu namna bora za kujilinda ambazo zinahamasishwa na shirika hilo.
Vita dhidi ya COVID-19 na utimizaji wa SDGs ni mitihani inayohitaji fedha:UN
Mkutano wa ngazi ya juu wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo umefanyika leo Alhamisi ukihusisha Umoja wa Mataifa na maafisa wawakilishi wa serikali mbalimbali, lengo kubwa likiwa ni kuchagiza msaada wa kimataifa wa fedha kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea ambazo zimedhoofishwa Zaidi na mlipuko wa janga la virusi vya corona au COVID-19 katika katika hatua zake za utumizaji wa malengo ya maendeleo endelevu , SDGs.
28 Mei 2020
-Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa :
-Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM la sema tushikamane kuchangia na kuwanusuru Wasyria na COVID-19
- Kuelekea siku ya walinda amani duniani kesho Mei 29, tunamulika askari wanawake wa Tanzania.
- Kutana na sajenti Desta anayesifika kwa kutengeneza magari ya UNMISS, Sudan Kusini
- Na kwenye Mashinani leo tutakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia jinsi mchungaji mwanaume alivyotumikishwa kingono na wanamgambo wanawake.
Kutana na Sajini Desta anayesifika kwa kutengeneza magari ya UNMISS, Sudan Kusini
Wanawake wanaohudumu katika shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa kote duniani wanaendelea kujizolea umaarufu kutokana na uchapakazi wao. Mmoja wao ni Almaz Kabtimer Desta, Sajenti anayefanya kazi katika Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNIMISS akihudumu kama fundi makenika.
Chonde chonde tushikamane kuchangia na kuwanusuru Wasyria na COVID-19:IOM
Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema fedha za ufadhili kwa ajili ya maelfu ya raia wa Syria waliotawanywa na machafuko inasalia kuwa kipaumbele kinachotia hofu kubwa ya utoaji msaada wa kibinadamu hasa wakati huu ambapo janga la virusi vya corona au COVID-19 linaongeza msumari wa moto juu ya kidonda.
COVID-19 ni tishio kubwa kwa raia waliokumbwa na mizozo:UN
Raia wasio na hatia ambao wamekwama katikati ya machafuko hivi sasa wanakabiliwa na tishio jipya kutoka kwa janga la virusi vya corona au COVID-19 , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la Usalama hii leo na kuonya kwamba janga hili janga hili linatumia fursa ya hali tete inayoikabili dunia.
Zaidi ya kijana 1 kati ya 6 hana ajira sababu ya COVID-19: ILO
Tathimini mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi duniani ILO kuhusu athari za janga la virusi vya corona au COVID-19 imedhihirisha hali halisi ya athari mbaya na kubwa katika ajira ya vijana na pia kuelezea hatua zinazochukuliwa kuhakikisha watu wanarejea salama katika mazingira ya kazi.
27 MEI 2020
Kwenya Jarida la Umoja wa mataifa hii leo
-COVID-19 yawa upenyo wa kutangaza maziwa ya kopo badala ya maziwa ya mama
-Tutasikia kauli ya mwandishi wa habari wa kujitegemea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na jinsi COVID-19 imebadilisha maisha ya familia yake.
-Pamoja na kuleta adha COVID-19 pia imekuwa faraja kwa wengine: tutasikia kutoka kwa Fundi Beatrice kutoka Tanzania anyeshona barakoa.
Pamoja na kuleta adha COVID-19 pia imenisadia silali njaa:Fundi Beatrice
Mlipuko wa virusi vya Corona au COVID-19 kwa kiasi kikubwa umeathiri kila nyanja ya maisha ya watu duniani kote ukiacha kwamba umesababisha mamilioni ya vifo lakini pia umeathiri uchumi na maisha ya kijamii.
COVID-19 yawa upenyo wa kutangaza maziwa ya kopo badala ya maziwa ya mama- Ripoti
Ripoti mpya ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau, inaonesha kuwa juhudi za kukomesha matangazo ya maziwa ya kopo kwa ajili ya watoto wachanga zinaendelea kukumbwa na mkwamo hasa wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.