Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia washikamana kwa wito wa fursa ya chanjo kwa wote dhidi ya COVID-19

Utafiti wa kutafuta Chanjo ya virusi vya Corona unaendelea
Unsplash
Utafiti wa kutafuta Chanjo ya virusi vya Corona unaendelea

Viongozi wa dunia washikamana kwa wito wa fursa ya chanjo kwa wote dhidi ya COVID-19

Afya

Zaidi ya viongozi wa kimataifa 150 leo wamezindua wito wa fursa kwa wote ya upatikanaji wa chanjo ya virusi vya corona au COVID-19 katika siku za usoni.

Viongozi hao wamesema “Hadi pale chanjo itaka[opatikana kwa wote ambayo msingi wake ni usawa na mshikamano , ndipo tutakapoweza kuwalinda watu wote na kuruhusu jamii kufanya kazi kwa usalama” hivyo muafaka wa kimataifa hauwezi kusubiri kusisitiza wito ambao unaainisha hali tete inayowakabili binadamu wote wakati huu wa janga la COVID-19.

Katika barua yao ya wazi viongozi hao wamezitaka serikali zote kuungana katika lengo la kusaka chanjo ya gonjwa hili la COVID-19.

Wito huo umekuja siku chache kabla ya mawaziri wa afya kukutana kwa njia ya mtandao kwenye Baraza la afya la dunia kikao cha 73 kinachotarajiwa kuanza Jumatatu ijayo Mei 18.

Viongozi hao wamesema “Lengo ni kuhakikisha kwamba chanjo ya COVID-19, upimaji na matibabu vinatolewa bure kwa kila mtu kila mahali. Fursa lazima zitolewe kwa wale wafanyakazi walio msitari wa mbele, watu walio katika hatari Zaidi nan chi masikini ambazo haziwezi kuokoa maisha.”

Wamesisitiza kuwa wakati dunia inakabiliwa na janga hili la COVID-19 itakuwa salama tu endapo kila mtu atakuwa na fursa ya kupata chanjo.

“Hii ni changamoto ya kimataifa ya kisiasa “wamekiri viongozi hao na kutoa wito kwa baraza la afya la dunia kufikia muafaka ambao utahakikisha fursa kwa wote ya upatikanaji wa chanjo na matibabu na kukumbusha kwamba mahitaji yana kipaumbele zaidi ya uwezo wa kulipia.

Chanjo bure kwa watu wote- Rais Cyril Ramapohosa

Mabilioni ya watu leo hii wanasubiri chanjo ambayo ni tumaini letu kubwa katika kutokomeza janga hili la COVID-19 amesema rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye amenukuliwa katika taarifa yake kwenye wito huo akisema “Kama nchini barani Afrika tumedhamiria kuhakikisha kwamba chanjo ya COVID-19 ni ya bure, kutengenezwa haraka na kusambazwa na bila gharama yoyote kwa watu wote. Asuala yote ya kisayansi yanapaswa kushirikiana baina ya nchi na hakuna mtu anayestahili kuachwa nyuma au kuwekwa mwisho kwenye orodha ya chanjo kwa sababu ya wapi wanakoishi au kwa sababu ya kipato chao.”

Rais Matamela Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo tarehe 25 Septemba 2018
UN/Cia Pak
Rais Matamela Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo tarehe 25 Septemba 2018

 

Viongozi hao wamaesema huu sio wakati wa kuchagiza maslahi binafsi au makampuni ya nchi Tajiri na serikali, au suala la kila mtu katika kuokoa maisha, au kuliacha suala hili la kimaadili na muhimu katika nguvu ya masoko. Kwa maslahi ya watu wote wa dunia viongozi hao wanachagiza upatikanaji wa chanjo na tiba.

“Hatuwezi kuacha mabwayenye , mashindano yasiyo na msingi na sera za utaifa ambazo zitakuwa kikwazo cha fursa za kiafya ziingilie suala hili muhimu.” Wameonya viongozi hao.

Katka barua hiyo iliyoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS na shirika lisilo la kiserikali Oxfam imeonya kwamba dunia haiwezi kumudu wachache kuhodhi kila kitu hali ambayo itakuwa kikwazo katika kufikia mahitaji ya fursa za afya kwa wote ili kuokoa maisha.

“Hili ni janga lisilo la kawaida na linahitaji hatua zisizo za kawaida kulikabili amesema Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf. “ Kupitia somo tulilolipata uhusu vita dhidi ya Ebola , serikali lazima ziondoe vikwazo vyote vya maendeleo na ufikishaji haraka wa chanjo na matibabu. Hakuna maslahi yaliyo muhimu Zaidi ya mahitaji ya kimataifa ya kuokoa maisha.”

 

Ellen Johnson Sirleaf,Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu kuhusu Uhamiaji wa kimataifa barani Afrika kwenye mkutano kuhusu uhamiaji Marrakesh, Morocco.
UN Photo/Mark Garten)
Ellen Johnson Sirleaf,Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu kuhusu Uhamiaji wa kimataifa barani Afrika kwenye mkutano kuhusu uhamiaji Marrakesh, Morocco.

Baraza la afya lakaribisha chagizo la chanjo kwa wote

Wakiunga mkono maneno ya mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel kutoka Liberia viongozi hao wamekumbusha kwamba wale ambao hawakumbuki yaliyopita basi wana hatari ya kuyarejea. “Lakini pia tunapaswa kukumbuka ushindi uliopatikana katika harakati za afya ikiwemo kazi kubwa ya watetezezi na wapigania haki wa vita dhidi ya ukimwi ambao walipambana kuwepo na fursa ya dawa za gharama nafuu kwa wote.”

Katika kuchagiza muafaka wa kimataifa viongozi hawa wa wanataka chanjo , upimaji na matibabu dhidi ya corona vitekelezwe chini ya uongozi wa shirika la afya duniani WHO.

Wamesema lengo kuu ni kuhakikisha ulazima wa kushirikiana ujuzi kimataifa, takwimu na teknolojia zinazohusiana na CIVID-19, kutoa leseni kwa nchi zote bila vikwazo. Nchi ziruhusiwe kutumia kwa uhuru makubaliano ya azimio la Doha  kuhusu haki miliki na makubaliano ya afya ya umma kulinda fursa za upatikanaji wa dawa kwa wote.

Pia linaanda mpango sawa wa utengenezaji na usambazaji ambao unafadhiliwa nan chi Tajiri kwa ajili ya chanjo. Kwa kifupi unahakikisha uwazi, gharama halisi na usambazaji kutokana na mahitaji. 

Lengo ni kuimarisha uwezo wa kimataifa katika kutengeneza mabilioni ya dozi za chanjo na kuwafundisha na kuwaajiri na kuwalinda mamilioni ya wahudumu wa afya ambao wwanahitajika kugawa au kutoa nchanjo hizo.

Miongoni mwa washiriki katika kampeni hii

Miongoni mwa watu Zaidi ya 150 waliotia Saini baria hiyo ni Pamoja na Rais wa Afrika Kusini Cyril ramaphosa, waziri mkuu wa Pakistan, Imran Khan, Rais wa Senegal Macky Sall na Rais wa Ghana Nana Addo Dankwa Akufo-Addo.

Wengine ni Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Gordon Brown, Rais wa zamani wa Mexico Ernesto Sedollo, Rais wa zamani wa Brazil Fernando Henrique Cardoso, waziri mkuu wwa zamani wa New Zealand Helen Clark na Raos wa zamani wa Ireland Mary Robinson.

Kundi hilo limeungana na wachumi mashuhuri duniani na wachagizaji wa masuala ya afya akiwemio mkurugenzi wa kituo cha Afrika cha kudhibiti magonjwa Dkt. John Nkengasong na mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa katika kutokomeza ufukara Olivier De Schutter na wa haki ya afya Dainius Puras.

Katika mfumo wa Umoja wa Mataifa amekuwepo pia mkuu wa UNAIDS Winnie Byanyima na Vera Songwe mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi kwa ajili ya Afrika ECA. 

Pia naibu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Loise Frenchette na Rais wa zamani wa Baraza Kuu Maria F. Espinosa. Wengine ni mkuu wa zmani wa UNICEF Carol Bellamy na mkuu wa zamani wa UNESCO Irina Bokova.