Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tathimini huru yahitajika dhidi ya hatua za WHO za kupambana na COVID-19: Azimio

WHO ilifikisha msada wa vifaa kinga dhidi ya COVID-19 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC mwezi Aprili 2020
WHO
WHO ilifikisha msada wa vifaa kinga dhidi ya COVID-19 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC mwezi Aprili 2020

Tathimini huru yahitajika dhidi ya hatua za WHO za kupambana na COVID-19: Azimio

Afya

Nchi wanachama 194  wa shirika la afya duniani WHO leo wamepitisha azimio  la kutaka tathimini huru ya hatua za kimataifa za kupambana na janga la virusi vya corona au COVID-19 . Tathimini hiyo itamulika natua za shirika la Umoja wa Mataifa WHO lakini pia sio peke yake.

Azimio hilo lililopitishwa le nan chi wanachama mjini Geneva Uswis limependekezwa na Muungano wa Ulaya wakati Baraza la afya Duniani likikunja jamvi.  Lengo kuu la azimio hilo ni kupata tathimini huru ya hatua za kimataifa katika kushughulikia janga la virusi vipya vya corona.

Azimio lililopitishwa na wanachama

Azimio hilo linasema “Maandiko haya yaliyopitishwa kwa muafaka bila kupingwa yanalenga kuanzisha uchunguzi haraka iwezekanavyo kuhusu chanzo cha VOVID-19 na hatua za kimataifa za kupambana na virusi hivyo. Itakuwa ni tathimini isiyoegemea upande wowote, huru nay a kina, tathimini ya hatua za kimataifa zilizorabitiwa na WHO katika kupambana na janga hili. Lengo pia ni kutathimini yale tuliyojifunza kutokana na hatua za kimataifa zilizoratibiwa na WHO wakati wa janga la COVID-19, kwa mtazamo wa kuboresha uwezo wa kimataifa kwa ajili ya kuzuia, maandalizi na hatua za kupambana na milipuko ya majanga kama hili.”

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus akizungumza katika moja ya taarifa za WHo kuhudsu janga la COVID-19
UN Photo/Evan Schneider
Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus akizungumza katika moja ya taarifa za WHo kuhudsu janga la COVID-19

Uchunguzi huo utabaini chanzo cha virusi na uwezekano wa njia za kusambaa kwa maambukizi hayo kwa binadamu. Kwa mantiki hiyo azimio hilo pia limeitaka WHO kushirikiana kwa karibu na shirika la afya ya mifugo duniani, shirika la chakula na kilimo FAO na nchi wanachama. Lengo ni kubaini Wanyama ambao ni chanzo cha virusi na kutambua ni jinsi gani virusi hivyo viliingia kwa binadamu.

Siku moja kabla mkurugenzi mkuu wa Who Dkt. Tedros Adhamon Ghebreyesus alisema thathmini hiyo huru kuhusu udhibiti wa janga la CIVID-19 unafanyika katika wakati muafaka lakini akaongeza kuwa “utaratibu huo unapaswa kujumuisha hatua za wadau wote kwa nia njema na kila nchi inapaswa kujifanyia tathimini  ya hatua zake na kujifunza kutokana na uzoefu huo.”

 

Muafaka wa haki ya chanjo nay a gharama nafuu

Katika Baraza hilo la afya nchi wanachama wa WHO pia wameafikiana kuhusu fursa ya siku za usono ya upatikanaji wa haki ya chanjo nay a gharama mnafuu.

Nchi zote 194 wanachama wameidhinisha azimio lisemalo kwamba furs azote za chanjo hapo baadaye na madawa mengine zitakuwa ni kwa ajili ya kila mtu kwa haraka na kwa haki ya ubora, usalama na gharama nafuu.

Katika ufunguzi wa Baraza hilo la 73 la afya  ambalo mwaka huu limefanyika kwa siku mbili tu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito wa haja ya juhudi za kimataifa na mshikamano dhidi ya janga la COVID-19 akitumai kwamba kusaka chanjo ya kutakuwa ndio mwanzo, na kusistiza kwamba kila mtu, kila mahali ni lazima awe na fursa ya huduma hizo.

Kwa kujibu wa takwimu za leo za WHO duniani kote kuna karibu wagonjwa milioni 4.7 wa corona na watu 315,131 wamepoteza Maisha kutokana na ugonjwa huo huku Marekani ikiongoza kwa vifo 89,272 na wagonjwa karibu milioni 1.5.

Inafuatiwa na Uingereza yenye vifo 34,636, Italia vifo 31,908, Ufaransa vifo 28,059 na Hispania vifo 27,650.