Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 ni tishio kubwa kwa raia waliokumbwa na mizozo:UN

Ulinzi wa raia ni agizo muhimu kwa shughuli nyingi za kulinda amani za Umoja wa Mataifa pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
UN Photo/Herve Serefio
Ulinzi wa raia ni agizo muhimu kwa shughuli nyingi za kulinda amani za Umoja wa Mataifa pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

COVID-19 ni tishio kubwa kwa raia waliokumbwa na mizozo:UN

Amani na Usalama

Raia wasio na hatia ambao wamekwama katikati ya machafuko hivi sasa wanakabiliwa na tishio jipya kutoka kwa janga la virusi vya corona au COVID-19 , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la Usalama hii leo na kuonya kwamba janga hili janga hili linatumia fursa ya hali tete inayoikabili dunia.

Antonio Guterres akitolea mfano vita kama moja ya sababu kuu za hali tete duniani katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video ukijikita na mada ya ulinzi wa raia katika maeneo yenye mizozo kwamba “virus vya corona vinasababisha zahma kubwa kwa binadamu na changamoto za ziada katika mifumo dhaifu ya afya , uchumi na jamii ambazo tayari zimedhoofishwa na miaka mingi ya vita.”

Amesema “COVID-19 sio tu kwamba inasambaza maradhi na vifo, pia inawatumbukiza mamilioni ya watu katika umasikini  na njaa na katika baadhi ya maeneo inabadili hatua kubwa zilizopigwa kwa miongo kadhaa.”

Wakati huohuo amesema wakati fursa za huduma zikiwa funyu na hatua kali zikichukuliwa na baadhi ya nchi kuwalinda walio hatarini Zaidi hususani katika maeneo yenye vita imekuwa vigumu sana.

Zaidi yah apo COVID-19 inatishia wakimbizi na wakimbizi wa ndaniwaliorundikana katika makambi na jamii ambazo zinakosa huduma muhimu za usafi na vituo vya afya.

Usitishaji uhasama kimataifa

Katibu Mkuu amekumbusha wito wake wa kimataifa wa usitishaji mapigano alioutoa mwezi Machi katika kupambana na janga hili akisema ingawa ulipokelewa vyema “lakini haujadhihirika kivitendo” na amesisitiza kwamba katika baadi ya maeneo janga la COVID-19 huenda ikasababisha ongezekeo la kipato kwa pande kinzani au kusahmbulia wakati mtazamo wa kimataifa hivi sasa ukiwa umejielekeza kwingineo.

Katibu amesema “Mazingira yote mawli yanaweza kusababisha ongezeko la machafuko na raia daiama ndio wanaolipa gharama kubwa.”

Akigeukia ulinzi wa amani mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amewaita wavaa kofia za blu za Umoja wa Mataifa kuwa ni moja ya njia muhimu zinazofanyakazi za kuwalinda raia katika maeneo yenye mizozo kote duniani. Amegusia msaada wao mkubwa kwa malaka za serikali kwa kulinda mifumo ya huduma za afya na wahudumu wa kibinadamu, lakini pia kuwezesha fursa za misaada na ulinzi.

Matarajio finyu

Kukiwa na hatua ndogo iliyopigwa katika kuzingatia sharia za kimataifa , zaidi ya 20,000 wamepoteza Maisha katika migogoro 10, maelfu ya watoto  waliingizwa vitani mwaka jana, mamilioni ya watu walitawanywa, wanawake na wasichana kukabiliwa na kiwango kikubwa cha ukatili wa kingono na kijinsia na vita kuwa ndio chanzo kikubwa cha njaa ya kimataifa.

Ameongeza kuwa ukatili dhidi wa wahudumu wa misaada na mali utalitawapa pia. Akitoa mfano amesema “shambulio la mwezi huu kwenye hospitali ya wazazi mjini Kabul ikiwa ni katikati ya janga la corona inafanya kuwa muhimu Zaidi kwa nchi wanachama kuchukua hatua za haraka kutekeleza maazimio ya Baraza la Usalama na kulinda vituo vya kutoa huduma za afya katika mizozo.”

Suluhu ya kisiasa ndio ufunguo

Akihitimisha taarifa yake kwa Baraza hilo Katibu Mkuu amesisitiza haja ya kuongeza juhudi kuzuia , kupunguza na kutatua migogoro lakini pia kuhakikisha uzingataji wa sharia za kimataifa na uwajibikaji.
“Suluhu endelevu ya kisiasa inasalia kuwa ndio njia pekee ya kuhakikisha raia wanabaki salama bila madhara”