Skip to main content

Kala Jeremiah anayesifika kwa nyimbo za kijamii, sasa aja na CORONA IPO.

Kala Jeremiah anayesifika kwa nyimbo za kijamii, sasa aja na CORONA IPO.

Pakua

Wakati mapambano dhidi ya virusi vya corona yakiendelea duniani kote, wito umekuwa ukitolewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kuwa ni jukumu la kila mtu kuwalinda wengine kama anavyojilinda hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaza elimu ya kutosha kwa jamii kuhusu namna bora za kujilinda ambazo zinahamasishwa na shirika hilo. Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Kala Jeremiah ambaye anasifika kwa kuimba nyimbo za kijamii, ametengeneza wimbo mahususi wa kuelimisha umma kuhusu hatua za kuchukua ili kujikinga na virusi vya corona, COVID-19, akienda mbali zaidi kuongelea madhara ambayo yanaweza yasitazamwe wakati wa mapambano dhidi ya ugonjwa huu ingawa yana madhara makubwa kwa mustakabali wa jamii nzima hususani watoto. Kupitia makala hii, kwa maneno yake mwenyewe, anaeleza kwa kina kuhusu wimbo huo CORONA IPO aliomshirikisha mwanamuziki mwenzake, Malaika.

Audio Credit
Loise Wairimu
Audio Duration
3'57"
Photo Credit
Picha: UNESCO